Katiba ya TFF ya 2012 ilifutwa na msajIli wa vyama vya michezo na vilabu kwa kuwa ilibadilishwa kinyume cha sheria(BMT)  pamoja na Katiba ya TFF ibara ya 30  kwa kutumia njia ya waraka badala ya Mkutano Mkuu,  hivyo katiba halali kisheria inayotambulika ni ile ya 2006 na mabadiliko yake . FIFA  na Serekali kupitia wizara yenye dhamana na  michezo iliiagiza  TFF iitishe Mkutano Mkuu ili ifanye mabadiliko ya katiba stahiki kwa mujibu wa katiba  na  kwa kufuata taratibu zilivyoainishwa  kwenye katiba ya TFF. Nimelazimika kuendelea kuiunga mkono Serikali kupitia  msajili  kwa maamuzi yake ya kukataa kusajili mabadiliko  ya katiba ya TFF kwa kuwa TFF  kwa makusudi   imeendelea kuvunja katiba yake katika kufanya mabadiliko.
Kisheria  msajili husajili mabadiliko yoyote ya Chama kilichosajiliwa chini ya Sheria ya BMT kwa kuzingatia  Sheria NA 12 ya 1967 na marekebisho yake NA 6 ya 1971 ya Baraza la Taifa la Michezo pamoja na  Kanuni za Baraza la Michezo la Taifa  na Kanuni za  Usajili NA 422 za1999.
 Chama chochote kitakacho kwenda kinyume na sheria hizo hikiwezi kupewa usajili au Katiba yake na marekebisho yake hayawezi kupewa usajili,aidha uamuzi wa msajili   sio tu utaifanya TFF peke yake itambue sheria  bali hata vyama vingine vitawajibika kufuata utaratibu katika kufanya mabadiliko ya katiba zao,
Katiba ni nyaraka ya kisheria hivyo chombo chenye mamlaka kisheria hapa Tanzania ya kutafsiri katiba ni Mahakama pale pande mbili zinapotofautiana juu ya tafssiri ya Katiba, hivyo kwa kufanya hivyo msajili atakuwa ameepusha suala la Katiba ya TFF kuingia katika mikono ya kimahakama kwa kuwa utaratibu uliotumika kubadili katiba ya TFF  ni dhahiri haukufuata taratibu zilizoainishwa kwenye katiba ya TFF  na sheria na  za nchi kama zilivyoaanishwa. Sababu kuu zinazonipelekea mimi kuunga mkono uamuzi huo ni kama zifuatazo:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...