Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu Augustino Ramadhani (aliyesimama) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara katika mkutano ulioitishwa na Tume ili kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya wakati wa mkutano uliofanyika Wilayani humo hivi karibuni. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Bw. Yahya Msulwa.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Mbeya, Bw. Tata Kibona akiwasilisha maoni ya wajumbe wenzake waliojadili eneo la maadili katika Rasimu ya Katiba Mpya iliytotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika hivi karibuni.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Bi. Salma Maoulidi (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoanMbeya  katika mkutano ulioitishwa Tume wa kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Tume, Profesa Mwesiga Baregu.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu (aliyeshika Rasimu ya Katiba Mpya) akzungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya katika mkutano ulioitishwa jana Jumanne (Agosti 13, 2013) na Tume hiyo ili kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume hiyo.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la Halmshauri ya Ilala, Mkoani Dar es Salaam Bi. Bi Margaret Ikongo akiwasilisha maoni ya wajumbe wenzake waliojadili eneo Muungano katika Rasimu ya Katiba Mpya iliytotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Arnatoglou Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wilaya ya mbozi mkoani Kilimanjaro????????

    ReplyDelete
  2. hiv jamani kwann watz hatupo makini na kazi zetu kweli kwenye mtandao mkubwa kama huu mtu unaandika wilaya ya mbozi mkoani kilimanjaro jamani sasa kwa mtu asiyejua hapa atajifunza nini, waandishi wetu tunawaomba muwe makini ktk kazi zenu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...