Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Said Mwema (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya (katikati) wakisaini hati ya ushirikiano wa kuchunguza matukio ya uhalifu kati ya Tanzania na Uturuki. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akilishuhudia tukio hilolililofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiwashukuru kwa furaha ujumbe kutoka nchini Uturuki baada ya kukabidhi gari maalumu ya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini kwa Jeshi la Polisi. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi akiliwasha gari maalumu la kuchunguza matukio ya uhalifu mara baada ya kukabidhiwa ufunguo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Uturuki, Zeki Catalakaya. Gari hilo ambalo linavifaa vyote vya kuchunguza matukio ya uhalifu nchini lilikabidhiwa leo Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (watatu kutoka kulia-waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe kutoka nchini Uturuki pamoja na maofisa wa Jeshi la Polisi nchini mara baada ya kusaini hati ya ushirikiano wa uchunguzi wa matukio ya uhalifu kati ya nchi ya Tanzania na Uturuki. Jeshi la Polisi Uturuki tayari limekabidhi ya gari maalumu la kuchunguza hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AHSANTE UTURUKI; WANAUZOEFU WA KUPAMBANA NA MILIPUKO YA MABOMU NA KUWAPATA WAHALIFU KWA MUDA MFUPI; NAWEZA KUSEMA NI WAZURI KULIKO FBI AU CIA. NAFIKIRI NI NCHI MOJAWAPO YA KUPATA ELIMU YA INTELIJENSIA KWA UZURI.

    ReplyDelete
  2. Msaada mzuri,serikali ifanye tathmini na kuongeza mengine kwani gari mmoja la kisasa kama hili katika masuala ya "security" halitoshi nchi nzima.

    ReplyDelete
  3. Gari itamtambuaje mhalifu kama gari yenyewe haikuwepo katika eneo la tukio?

    ReplyDelete
  4. Yetu macho na masikio,Tunasubiri ili tuseme.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...