
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana kutoka Taasisi ya MitoSt ya Hamburg Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia ushitikiano wao wa kubadilishana rasilimali watu na kujitolea kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition (TYC) walipotembelea Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo wageni hapo wamekuja na ujumbe mahususi wa furaha kwa wote.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana wanaojitolea kutoka Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia mpango wao wa kubadilishana rasilimali watu kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizarani hapo.
Afisa Mipango wa MitOst Mete Odabasi akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kwa niaba ya Wizara ya Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo kufuatia ushirikiano waliopewa katika ziara yao hapa nchini.

Mmoja wa wanachama wa Tanzania Youth Coalition (TYC) ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bibi Neema Kassala (kushoto) akichangia mada walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo yaVijana walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam kufuatia kuwa wenyeji wa wageni kutoka Taasisi ya MitoSt ya jijini Hamburg Ujerumani waliopo nchini.

Mmoja wa wakilishi kutoka Taasisi ya MitOst yenye makao yake jijini Hamburg Ujerumani Bibi Lusinja Czesnik (wa pili kutoka kushoto) akichangia mada jana walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya kitamaduni kutoka kwa Afisa Mipango wa taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani Mete Odabasi walipokutana na Mkurugenzi huyo Jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.


Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana na wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza nama Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Frank Shija wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo



Makubwa ya kujifunza kwa Vijana wa Kijerumni:
ReplyDeleteVijana wa Kitanzania mtafute yafuatayo kwa hao wenzenu wa Ujerumani,
1.Kujituma na Uwajibikaji,
2.Umakini na kujali muda ktk mambo,
3.Uwazi na ukweli,
4.Ubunifu na Utafutaji,
5.Kijali maslahi ya nchi zaidi (Uzalendo)
Ngoja ifike zamu ya watanzania kwenda ujerumani tuone ubalozi wa ujerumani utavyoanza kuleta roho mbaya katika swala la VIZA
ReplyDeleteWachungeni sana wale jamaa wa "tindikali"..Ohooo
ReplyDeleteWalitumia Lugha gani katika kuwasiliana hapo?
ReplyDeleteMdau wa pili,je ulishawahi kusafiri ujerumani? Au umaendika tu?nimeenda ujerumani mara kadhaa na hawasumbui kwenye visa kama sababu inaeleweka hawana tabu kabisa. Nadhani wako better kuliko balozi zingine mana nimesafiri nchi kadhaa. Kama unaenda kwa kualikwa au kumuona ndugu kweli unaweza pata shida kidogo ila kama ni workshop, chuoni au kikazi hakuna tatizo kabisa. Napiga hoja yako. Wako very friendly tena nilisafiri kwenye workshop yule mama akasema hata ukipenda kuongeza siku week 2 zaidi hakuna neon baada ya workshop kuisha mie nikamwmabia hapana nina mana nina majukumu mengi ya kazi nikirudi Tz.
ReplyDeleteme nimoja kati ya hao vijana tulioenda ujeruni. nashukuru mdau wa kwanza kwa ushauri wako na pia hayo ndiyo mambo ambayo me binafsi nilizingatia pamoja na wenzangu pia. na kwenye swala la viza hata haikuchukua wik tulipata ndani ya wiki bila tatizo lolote na kwenye lugha ya mawasiliano tulitumia kingereza sababu kuna wajeruman pia wanaongea kingereza ingawa wengine hawakijui.
ReplyDeletena mambo ya msingi vijana wenzangu wa kitanzania ni kuzidi kuwa na ushirikiano kati yetu na kujivunia sana utamaduni wetu sababu hata sisi tulivyoenda ujerumani hayo mawili ndo yalikuwa identification yetu na hata kufanya wenzetu wajeruman wajifunze mengi