Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana kutoka Taasisi ya MitoSt ya Hamburg Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia ushitikiano wao wa kubadilishana rasilimali watu na kujitolea kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition (TYC) walipotembelea Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo wageni hapo wamekuja na ujumbe mahususi wa furaha kwa wote.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana, wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na vijana  wanaojitolea kutoka Ujerumani ambao wapo nchini kufuatia mpango wao wa kubadilishana rasilimali watu kupitia asasi ya kirai ya Tanzania Youth Coalition jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizarani hapo.
 Afisa Mipango wa MitOst  Mete Odabasi akitoa neno la shukrani kwa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kwa niaba ya Wizara ya Habari. Vijana, Utamaduni na Michezo kufuatia ushirikiano waliopewa katika ziara yao hapa nchini.
 Mmoja wa wanachama wa Tanzania Youth Coalition (TYC) ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bibi Neema Kassala (kushoto) akichangia mada walipokutana na Mkurugenzi wa  Maendeleo yaVijana walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam kufuatia kuwa wenyeji wa wageni kutoka Taasisi ya MitoSt ya jijini Hamburg Ujerumani waliopo nchini.
 Mmoja wa wakilishi kutoka Taasisi ya MitOst yenye makao yake jijini Hamburg Ujerumani Bibi Lusinja Czesnik (wa pili kutoka kushoto) akichangia mada jana walipokutana na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana leo jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Prof. Elisante Ole Gabriel akipokea zawadi ya kitamaduni kutoka kwa Afisa Mipango wa taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani Mete Odabasi walipokutana na Mkurugenzi huyo  Jana jijini Dar es Salaam walipotembelea Wizara ya Habari, Vijina, Utamaduni na Michezo ili kujifunza namna Serilikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya vijana hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo  jana jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na baadhi wafanyakazi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana na wawakilishi kutoka taasisi ya MitOst ya jijini Hamburg Ujerumani walipotembelea Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kujifunza nama Serikali ya Tanzania inavyoshughulikia masuala ya Vijana kupitia wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam. Picha Zote na Frank Shija wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Makubwa ya kujifunza kwa Vijana wa Kijerumni:

    Vijana wa Kitanzania mtafute yafuatayo kwa hao wenzenu wa Ujerumani,

    1.Kujituma na Uwajibikaji,
    2.Umakini na kujali muda ktk mambo,
    3.Uwazi na ukweli,
    4.Ubunifu na Utafutaji,
    5.Kijali maslahi ya nchi zaidi (Uzalendo)

    ReplyDelete
  2. Ngoja ifike zamu ya watanzania kwenda ujerumani tuone ubalozi wa ujerumani utavyoanza kuleta roho mbaya katika swala la VIZA

    ReplyDelete
  3. Meku-UghaibuniAugust 14, 2013

    Wachungeni sana wale jamaa wa "tindikali"..Ohooo

    ReplyDelete
  4. Walitumia Lugha gani katika kuwasiliana hapo?

    ReplyDelete
  5. Mdau wa pili,je ulishawahi kusafiri ujerumani? Au umaendika tu?nimeenda ujerumani mara kadhaa na hawasumbui kwenye visa kama sababu inaeleweka hawana tabu kabisa. Nadhani wako better kuliko balozi zingine mana nimesafiri nchi kadhaa. Kama unaenda kwa kualikwa au kumuona ndugu kweli unaweza pata shida kidogo ila kama ni workshop, chuoni au kikazi hakuna tatizo kabisa. Napiga hoja yako. Wako very friendly tena nilisafiri kwenye workshop yule mama akasema hata ukipenda kuongeza siku week 2 zaidi hakuna neon baada ya workshop kuisha mie nikamwmabia hapana nina mana nina majukumu mengi ya kazi nikirudi Tz.

    ReplyDelete
  6. me nimoja kati ya hao vijana tulioenda ujeruni. nashukuru mdau wa kwanza kwa ushauri wako na pia hayo ndiyo mambo ambayo me binafsi nilizingatia pamoja na wenzangu pia. na kwenye swala la viza hata haikuchukua wik tulipata ndani ya wiki bila tatizo lolote na kwenye lugha ya mawasiliano tulitumia kingereza sababu kuna wajeruman pia wanaongea kingereza ingawa wengine hawakijui.

    na mambo ya msingi vijana wenzangu wa kitanzania ni kuzidi kuwa na ushirikiano kati yetu na kujivunia sana utamaduni wetu sababu hata sisi tulivyoenda ujerumani hayo mawili ndo yalikuwa identification yetu na hata kufanya wenzetu wajeruman wajifunze mengi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...