Muonekano wa choo hicho kwa mbele kutokana na kukosa milango wamelazimika kutengeneza uzio wa nyasi.
Kushoto ndiyo tundu halisi la choo, na tundu la kulia limetokana na choo hicho kubomoka chenyewe.

 Nyufa zilizomo kwenye kuta za choo hicho.

=============================
Na Edwin Moshi, Makete.

Wanafunzi wa shule ya msingi Uganga kata ya Luwumbu wilaya ya Makete mkoani Njombe wapo hatarini kupoteza maisha yao kutokana na vyoo wanavyovitumia kubomoka na kuweka nyufa na matundu makubwa kutokana na uchakavu.

Mtandao huu umebisha hodi shuleni hapo hivi karibuni ka kukuta vyoo hivyo vinavyotumiwa na wanafunzi vikiwa katika hali mbaya huku wanafunzi hao wakiendelea kuvitumia bila wasiwasi.

Mwanafunzi mmoja anayesoma darasa la tano katika shule hiyo ambaye hakupenda jina lake liandikwe mtandaoni amesema haoni shida kutumia vyoo hivyo kwa kuwa hakuna sehemu nyingine ya kujisaidia na kuongeza kuwa licha ya hatari ya kupoteza maisha waliyonayo wanafunzi wanaotumia vyoo hivyo lakini bado wataendelea kuvitumia.

Akizungumzia suala hilo mwalimu mkuu wa shule hiyo Eliuda Danie Kyando amekiri kuwepo kwa vyoo hivyo chakavu na kusema kuwa ameshapeleka kwenye ngazi husika suala hilo ambapo amejibiwa kuwa litafanyiwa kazi.

Amesema kwa hivi sasa wanamuomba Mungu isitokee hatari yoyote kwenye vyoo hivyo katika kipindi hiki wanaposubiri wakubwa kulishughulikia suala hilo kama walivyomuahidi ingawa ni muda mrefu umepita.

"Mimi katika taarifa zangu wakati mwingine huwa naandika kuwa shule haina vyoo vya wanafunzi kutokana na uchakavu hebu ona mwenyewe vyoo gani hivi, hii si hatari tupu, matundu mengine tumeziba na magogo ili wanafunzi wasiingie" alisema.

Shule hiyo ambayo inadhaniwa kuanza miaka ya 1970 inakabiliwa na changamoto lukuki ikwemo majengo kwa kuwa mengi yamechakaa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mbona vyoo vizuri tu hivi, mngeona vyoo vyetu huku Washington wala msingethubutu kutoa hizi picha.

    ReplyDelete
  2. Wanaohusika washughulikie jambo hili

    ReplyDelete
  3. hapo mtu unakula kabisa bila wasiwasi Hongera TANZANIA KWA MIAKA YA UHURU

    ReplyDelete
  4. Kisheria hiyo shule inabidi ifungwe kabla ya kusingizia kazi ya Mungu haina makosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...