Jumla ya wahamiaji haramu 8509 kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Uganda wameondoka nchini kwa hiari yao baada ya agizo la Mh. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete lilitolewa hivi karibuni akiwa ziarani mkoani Kagera.
Wahamiaji hao haramu wametoka katika mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma.
Kati ya hao wahamiaji haramu 5521 wamerudi nchini Rwanda, 2744 wamerejea kwao nchini Burundi na 244 warejea kwao nchini Uganda. Katika zoezi hilo siraha zipatazo 60 zimerejeshwa kwa hiari zikiwemo siraha aina ya SMG na Magobole.
Aidha, zoezi hilo la kuwarejesha wahamiaji haramu limekwenda sanjari na urejeshaji wa mali na mizigo ikiwemo jumla ya mifugo 1996 iliyorejeshwa katika nchi za Rwanda, Burundi na Uganda.
Serikali inapenda kusisisitiza kwamba imefurahishwa sana na ushirikiano iliyouliopata kutoka nchi za Rwanda, Burundi na Uganda hasa katika kuwapokea wahamiaji hao haramu na kushirikiana na Tanzania katika zoezi hilo.
Aidha , katika zoezi hilo idadi ya wahamiaji haramu waliondoka ni kwa hiari na Serikali inawasihi wahamiaji haramu ambao bado wako nchini kuondoka haraka iwezekanavyo kabla ya hatua ya kuwaondoa kwa nguvu hazijaanza.
Zoezi la kurejea kwa wahamiaji haramu ni utekelezaji wa agizo la Rais Jakaya Kikwete, alipotoa siku 14 kwa wahamiaji kuondoka nchini kwa hiari ndani ya kipindi hicho.
Imetolewa na Idara ya Habari(MAELEZO)
15 Agosti, 2013
Hongera Serikali kwa maamuzi Magumu kunamsemo usemao mchelea mwana kulia atalia mwenyewe. Tuiunge serikali mkono katika utekelezaji wa maamuzi haya ambayo ni kwa manufaa yetu sote. Tuache kulalamika pasi kujua kwa nini serikali imeamua kufanya hivyo. Mungu ibariki Tanzania na Watu wake
ReplyDeleteWASHINGTON (Reuters) - Former Illinois congressman Jesse Jackson Jr., once one of the most promising black politicians in the United States, was sentenced on Wednesday to 2-1/2 years in prison for misuse of campaign funds.
ReplyDeleteHis wife, Sandi, a former Chicago city council member, was sentenced to one year for falsifying tax returns that failed to report the campaign money as income.
Raisi wetu tunaomba mambo haya yawepo bongo,viongozi walarushwa na wanaotumia mali za walipa kodi wawajibishwe kama huyu jamaa.
Wahamiaji haramu ni wale ambao hawana makaratasi yakuishi katika nchi. Hii ikiwemo wale waliokataliwa kuishi nchi fulani au wameingia bila ya idhini ya nchi husika. Watu waliomba hifadhi ya kisiasa au wakimbizi sio wahamiaji haramu.
ReplyDeleteNa wasirudi tena,maana tumewalea vizuri hadi wakaanza kuona na kuzaliana utafikiri wako kwao,halafu wanatulipa matusi kwa rais wetu
ReplyDeleteTZ tusipende sana kulitumia jina la Raia haramu tafuteni jina lingine! Hao ni Watu pia. Haramu haramu jamani chondechonde!.
ReplyDeleteMnaomba chanzo cha Ujambazi hicho?
ReplyDeleteAngalieni tulikuwa tumewadhamini watu kukaa kama Wakimbizi kumbe kibindoni wana Mabunduki kama SMG!
Hongera Raisi Kikwete kwa maamuzi magumu,
Kuna msemo usemao HURUMA ISIZIDI UWEZO!!!
UWEZO WETU KUWAFUGA MAJAMBAZI UMEKOA HAPA NA MKUBWA WETU AMESHATOA MAAMUZI.
Kagame pokea hao wageni!
ReplyDeleteMbona Wachina wanaofanya biashara za mama ntilie ,mechanic na maduka hawajaondoka? Tunaomba serikali iwachukulie hatua kama hawa ndugu zetu wa karibu.Itakuwa ni vibaya sana tukiwaacha wachina wakifanya wanavyotaka hapa nchini kwetu na kuwafukuza ndugu zetu amabao waliweka makazi ya kudumu.
ReplyDeleteHili litamaliza matatizo ya Tanzania,ujambazi,uhaba wa maji,elimu,rushwa,chuki za kidini,uongozi wa kimbulula.hongera mwanakwetu jakaya.
ReplyDeleteWee anony unaowasema wachina hovyo kabisa..hivi unawajua wanyarwanda wewe...hao wakihamia sehemu baada ya muda wanadai ni kwao mfano mzuri hao wakongo c wameng'ang'ania sasa utasema kwao...wachina wakizidi kuwatimua easy sio hao banyamulenge..hatariii...EAC tuikatae kwa nguvu zote maana moja ya lengo lao ni hilo kujitanua tu hawana lolote hao rwanda..tunamshukuru kagame kumtusi kwake mh rais wetu kumetufungua masikio....na waende salama hatuwahitaji kwa kitu chochote uharibifu tuu.
ReplyDelete