Mjumbe wa Baraza la Katiba la
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Hassani Mkivanga (aliyesimama)
akiwasilisha maoni kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya
Mabadiliko ya Katiba mbele ya Wajumbe wa Tume hiyo kutoka kulia Bi. Kibibi
Hassan, Joseph Butiku na Mjumbe wa
Sekretarieti ya Tume, Bw. Mubarak Saleh. Mkutano huo ulifanyika jana Jumatano
(Julai 31, 2013) katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo
Wilayani humo.
Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Bw. Joseph Butiku akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Katiba la
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro (hawapo pichani) wakati wa
kufunga mkutano wa Baraza hilo jana Jumatano (Julai 31, 2013) katika ukumbi wa
Chuo cha Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo. Kulia ni Mjumbe wa Tume
hiyo, Bi. Kibibi Mwinyi Hassan.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bi. Christina Kasaga
akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili na kuitolea maoni Rasimu ya
Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha
Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo jana Jumatano (Julai 31, 2013).
1.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la
Halmashauri ya Wilaya yua Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Thomas Edward
akichangia akichangia hoja wakati wa mkutano wa kuijadili na kuitolea maoni
Rasimu ya Katiba Mpya iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha
Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo jana Jumatano (Julai 31, 2013).
1.
Mjumbe wa Baraza la Katiba la
Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Bw. Hamza Mwanga
akiwasilisha maoni ya wajumbe wa kundi lake kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya
iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Chuo cha
Ualimu cha Green Bird kilichopo Wilayani humo jana Jumatano (Julai 31, 2013). Picha na Tume ya Katiba
pls can u give me details of how i can get this constitution of Tanzania both new and old,and i want to know why its very hard for we locals citizens to get Katiba yet we are the ones who should be given first priority.Tume ya katiba you should do something.
ReplyDelete
ReplyDeleteSilas, ungekuwa M-Tanzania ungepata Katiba zote ili uzichambue na kutoa maoni yako kwa faida ya nchi yetu, lakini kwakuwa wewe siye, jitahidi na wewe upate mchakato na rasimu ya katiba ya nchi yako ulikotoka utoe maoni yako kwa faida yako na wananchi wa nchi yako. Habari ndiyo hiyo!
Kama Silas umeweza kuingia michuzi kwanini iwe shida kupata katiba ya nchi, ingia kwenye website ya serikali utaona
ReplyDelete