Mkazi wa Makumbusho Isabela Edwad Msemo akipokea funguo ya Bajaji akiwa mwenye furaha kutoka kwa Meneja Chapa wa Tigo, Wiliam Mpinga mara baada ya kujishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam.
Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akipokea funguo za Bajaji mpya aliyojishindia kupitia
Promosheni ya Miliki Biashara yako na tTgo kutoka kwa Meneja Chapa wa
Tigo Wiliam Mpinga ambapo washindi wa wiki ya pili ya Promotion hiyo
wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam.
Evelyn Elisalia Massawe-(22) Mkazi wa Kimara akishuka ndani ya bajaji yake aliyokabidhiwa na Tigo baada ya kujishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo, kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.
Mkazi wa Mabibo Khalid Jafari Gomani akikagua Bajaji mpya aliyojishindia kupitia Promosheni ya Miliki Biashara yako na Tigo ambapo washindi wa wiki ya pili ya wamekabidhiwa zawadi zao jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Chapa wa Tigo Wiliam Mpinga.
Si kumpa Bajaj tu, hakikisheni anayo leseni halali kabla hajaingia njiani isje kuwa majanga.
ReplyDeleteHiyo promotion ni watu wa DSM tu.Huwa kuna jambo moja silieelewi, promotion zilizo nyingi hasa za mitandao ya simu washingi wengi hutokea DSM...ni kwa nini? au mikoani watu hawachangakii hizi fursa...
ReplyDeleteDuhhh kweli tiGO mmefanya kweli!
ReplyDeleteKwa kweli wasichana wamejikomboa na upandaji wa mabasi na kudhalilika kwa Lifti za watu wenye mashariti magumu.
Kibongo Bongo umiliki wa Bajaji si haba.
Mdau wa Kwaqnza umenena,
ReplyDeleteLingine zaidi ya Leseni halali ni vipimo vya Kiafya kama Macho, Magonjwa ya Kiasili au ya kuzaliwa na Netiwork zao vichwani!
Ni ajabu na kweli Dunia nzima Tanzania ndio nchi pekee haina utaratibu wa kuwapima Madereva afya zao mara kwa mara.
Bongo Jambaland, Bongotambarale ukishapewa Gamba au Leseni ndio imetoka milele na milele, hata kama utapata Utaahira ahalan wasalan utakaa barabarani ukiendesha gari weee hadi siku Kichwa kitakapo panda moto zaidi utakapokuwa hushikiki kwa Uchizi ndio utany'anganywa Funguo za gari!
Mbona mshindi ni mrembo sana!
ReplyDeleteNi jambo la muhimu sana mdau amegusia kuhusu kupima madereva afya zao (hasa afya za akili) kaka michuzi kwa nini usite hii kwenye globu ijadiliwe?mimi nadhani unaweza kutumia forum hii kufikisha maoni ya wananchi juu ya baadhi ya kero,ukizangatia kwamba mitandao hii sasa inatambulika. Iweke hii tujadili,ajali zinatokea wakati mwingine kwa kuwa madereva wameshabaki tu na leseni ila wamepoteza sifa zote za udereva,mfano kuona, akili timamu nk.
ReplyDelete