Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno Mteta, akionesha sehemu ya madini yaliyokamatwa.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno Mteta, akifafanua jambo. Kushoto ni Ofisa habari wa TMAA, Mhandisi, Yisambi Shiwa.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno Mteta, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu madini yaliyokamatwa. wa pili kushoto ni Ofisa habari wa TMAA, Mhandisi, Yisambi Shiwa na kulia ni Mkurugenzi wa Uthamini Madini na Huduma za Maabara, Mhandisi, Rwekaza Dominic.
---
Na Irene Mark
WAKALA wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) umekamata shehena ya madini yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 13 katika kipindi cha miezi 10 iliyokuwa ikitoroshwa nchini kinyume cha utaratibu.
Madini hayo yalikamatwa kwenye viwanja mbalimbali vya ndege hapa nchini ambapo wakaguzi wa TMAA kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji, Usalama wa Taifa, watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Jeshi la Polisi na wafanyakazi wa viwanja vya ndege (TAA).
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za wakala huyo jijini Dar es Salaam jana , Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno Mteta alisema madini hayo yalikamatwa kati ya Septemba mwaka 2012 na Julai mwaka huu katika matukio 23 tofauti.
Alisema kwa mwezi huu tayari wakala huyo umewakamata raia wawili wa kigeni wakiwa na shehena ya madini wakitaka kutoroka nayo huku akisisitiza kwamba watapandishwa kizimbani wakati wowote.
“Agosti 20 mwaka huu tumewakamata raia wawili wa kigeni mmoja alikuwa anasafiri amekamatiwa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA) akiwa na madini ya vito yenye thamani ya sh milioni 25.32.
“…Wa pili amekamatwa akiwa kwenye makazi yake Jangwani Beach hapa jijini kwa kweli thamani ya madini ya mtuhumiwa huyu hayakutambukuka,” alisema na kuongeza kuwa serikali imeyataifisha madini hayo.
Kwa mujibu wa Mteta wafanyabiashara wa kigeni na wazawa wanaruhusiwa kusafirisha madini hayo kwa kuzingatia utaratibu ili serikali ipate mgao wake huku akisisitiza kwamba serikali inategemea mapato ya madini kujiendesha.
Awali mkurugenzi huyo alisema tangu mwaka 2009 hadi mwishoni mwa mwaka jana serikali imepokea sh bilioni 317.74 ambazo ni mrabaha uliolipwa na kampuni 10 kubwa za madini hapa nchni.
Alisema hivi sasa wizi wa madini kwenye migodi mikubwa haupo kutokana na uwepo wa watumishi wa TMAA wanaotoa ripoti ya uzalishaji kila siku na kwamba wafanyabiashara wa madini wanaoongoza kwa kukwepa kodi ni wazawa.
Mteta alieleza changamoto zinazoukabiliwa wakala huyo kuwa ni kushindwa kuifikia mipaka yote inayounganisha nchi jirani (njia za panya) ambazo hutumika na wafanyabiashara wengi kutorosha madini hayo.
Alisema watoroshaji wengi wa madini hayo ni wageni kutoka nchi mbalimbali ambao wanauziwa madini na watanzania na kufafanua kwamba kati ya matukio 23 watanzania wawili.
Mkurugenzi huyo alisema tayari kesi tatu kati ya 23 zimesikilizwa na kutolewa hukumu na kutoa mfano wa kesi ya mgeni aliyekamatwa na madini yenye thamani ya zaidi ya Dola 6,200 za Marekani alitozwa faini ya sh milioni 1.5 na madini yake kutaifishwa na serikali.


The fine is peanuts to a mineral export. Sheria ni soft sana jamani. Na ndio mishahara ya watu kama wahudumu wa pale airport midogo. Lazima sehemu nyet kama hizi zipewe motisha ya kutosha ili wasiingie vishawishi. Hapo mnapotueleze ni kwamba yameshapita madini ya mabilioni na hakuna aliekamatwa. Huyu inaelekea ameshazoweya kupitisha. Asingesubutu kuweka madini mengi namna hiyo katika chupa na kusafiri nayo bila ya wasiwsi kwa mkupuo. Lazima kuna wtanzania wanahsika. Jamani msitutie changa la macho.
ReplyDeleteJamani hii ni hatali kubwa,hivi kwanini mgeni tena mwizi wa mari zetu apigwe faini? Kwanini asinyongwe iwe fundisho kwa wengine,hii ni aibu kubwa sn kitaifa na kimataifa yaani nchi inachezewa kila idala mara midawa ya kulevya midini inatoloshwa mbugani nako ndio usiseme jamani hivi ni nini maana ya kuwa na jeshi la POLISI au mgambo? Au nini maana ya wizara ya mambo ya NDANI? Hii wizara ingevunjwa jamani ili iundwe upya kabla nchi yetu kutekwa,uzaifu wa hii WIZARA ipo siku italeta janga kubwa kwenye hii nchi,eti nchi yetu ni vigumu kuifikia MIPAKA YAKE YOTE,hii kauli mm imenikatisha tamaa kabisaa yani uwe na nyumba ushindwe kuilinda? Hiki ni kioja jamani,,mm naona huu ni muda muafaka wa kutumia jeshi letu tukufu la JWTZ sehemu zote nyeti kama viwanja vya NDEGE,MBUGA ZA WANYAMA,MABANDARI YOTE,na MIPAKA YOTE YA NCHI YETU,mfano SOUTH AFRICA kona zote za nchi yani mipakani inalindwa na jeshi lao,mwende huko mkajifunze jamani,naitwa mdudu KAKAKUONA mwenye macho ma3 ASANTENI sn ndugu zangu watz,hayo ni mawazo yangu kwenye nchi yangu,au nyinyi mwaonaje wenzangu?
ReplyDeleteJukumu la ulinzi wa mipaka ya Tanzania si lenu nyie kama Taasisi, hiyo ni kazi ya watu na wanaeleweka,wananchi wanaweza wakawa wasaidizi tu.
ReplyDelete