
WanaDMV Jumapili Aug 18, 2013 kuanzia saa 11 jioni tutaanza mazoezi rasmi Meadowbrook Park kama kawaida na hii ni baada ya kumalizika kwa mfungo wa mwezi wa Ramadhani na Wazee wameomba mechi ya marudianoi na Vijana Jumapili Aug 25, 2013 lakini kwa masharti kwamba mtanange upigiwe Meadowbrook na sio Heurich Field kwa sababu Wazee mapafu yao hayana hewa ya kutosha kufukuzana na Vijana pili uwanja wa Meadowbrook ni uwanja waliouzoea pia wanabahati nao kuwasurubisha vijana.
Tafadhali tuzingatie muda na upatapo taarifa hii mtaarifu na mwenzio asante
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...