Mama mwenye hasira wa mmoja wa wasichana wa Uingereza waliomwagiwa acid mjini Zanzibar ameungana na bintiye nchini humo baada ya jana kuwasili kwa ndege kwenye hospitali kwa ajili ya matibabu.

Mama huyo, Nicky Gee alionekana kushindwa kujizuia kulia baada ya kumuona binti yake Katie na rafiki yake Kirstie Trup wakishuka kwenye ambulance akiwa amefunikwa blanket.

Wasichana hao ambao wote wana miaka 18 walipelekwa kwenye hospitali ya Chelsea and Westminster kutibiwa haraka majeraha ambayo baba yake Katie ameyaita mabaya yasiyoelezeka.


Wote wameungua vibaya baada ya kumwagiwa tindikali usoni wakati walipokuwa wakiingia kwenye mgahawa mjini Zanzibar.
Hilo lilikuwa shambulizi la tatu wakati walipokuwa visiwani humo. Awali mmoja wa wasichana hao alishambuliwa na msichana wa kiislam baada ya kumsika akiimba wimbo wakati wa mwezi wa Ramadhan.

Katie na Kirstie
Polisi wamedai kuwa washukiwa saba akiwemo muongozaji wa watalii wamekamatwa jana asubuhi.Na sasa zawadi ya paundi £4,000 imetangazwa kutolewa na polisi Zanzibar kwa atakayesaidia kupatikana kwa kwa wahalifu hao.
Marafiki wanadai kuwa walikuwa wamelengwa kushambuliwa kwasababu walikuwa ni wayahudi na polisi wanadai kuwa walikuwa wanataka kuongea na mhubiri wa kiislam ambaye huenda ndiye alipanga shambulizi hilo.
Polisi wamedai kutoa warrant ya kukamatwa kwa Sheikh Issa Ponda Issa, ambaye inasemekana mafundisho yake yamechochea mashambulizi hayo ya tindikali.
Wasichana hao watapata matibabu ya kina kutokana na mejeraha waliyoyapata kwa kumwagiwa tindikali hiyo iliyomwagika usoni, kifuani, miguuni na mgongoni.

Mikono yao pia imejeruhiwa kwakuwa walikuwa wakijaribu kufuta tindikali hiyo. Baba yake na Miss Trup, Marc, 51, milionea na daktari wa meno alisema mpita njia alienda kuwasaidia wasichana hao baada ya kushambuliwa na alimpigia simu.
Marafiki hao walikuwa wameenda Zanzibar kama walimu wa kujitolea kwenye kituo cha watoto yatima. Tukio hilo linaweza kuathiri vibaya sekta ya utalii visiwani Zanzibar.
hawa waliofanya vitendo hivi wapewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine , wanaitukanisha zanzibar na watu wake, washenzi sana sana
ReplyDeleteMzee Michuzi, Nchi hii ni yetu sote sasa Naomba mfungue njia na sisi tunaokaa nje ya nchi tuwasaidie kuwakamata wote wasio penda amani ya Tanzania.
ReplyDeleteMckenzie
Blog ya jamii,sikubaliani na hivi vitendo vya kihuni hata kidogo lakini nimekuwa nikisoma humu kwenye blog(kwa muda mrefu) vijana wa kitanzania na hasa walioko masomoni huko ng'ambo,wakiuawa kinyama na dunia 'hailaani'.Why are these girls treated so special?BINADAMU WOTE NI SAWA....
ReplyDeleteDavid V
waachiewe hiyo zanzibar yao kwanza chafuu imejaa magofu kila kona jina lina mvuto ila kiukweli wala si pazuri mombasa iko juu kuliko hicho kizanzibar chenu kilichojaa udini deile. mnalazimisha kila mtu afate dini yenu kwani lazima. halafu nyie wazenji mlivyojazana uingereza utazani unguja mngekaa kwenu pachovu kama nini. dubai huko ndo kwenye waisilam haswa lakini hamna upuuzi kama wenu na watu wanavaa watakavyo hujasikia huu upuuzi wenu ukitokea mnajidai mnaijua dini kuliko waarabu waliyowaletea hiyo dini. shikeni adabu nyie na ngoja utalii ufe huko ndo mtatia akili. muende saud arabia mkachukue waarabu wenzenu waje washangae hayo magofu yenu machafu. mmeiaibisha nchi kwa ajili ya ujinga wenu.
ReplyDeleteDavid, two wrongs never make one right. Nakushangaa kama una maanisha vile kuna uovu unaofanyika duniani, then it is okay uovu zaidi kufanyika. Forget for the time being kwamba wasichana waliomwagiwa tindikali walkuwa watalii. Wale wasichana a angeweza kuwa binti zako, dada zako, binamu, rafiki zako. How woulld that make you feel?! Usingejali kwa vile maovu mengi yanayotokea duniani? The girls had full of plans and dreams of life ahead of them. And they were there for a good cause, helping the people. Their dream is shattered by few evil people. Wazanzibari pingeni huu uovu kwa nguvu zote. Watajeni waliohusika na hivi vitendo. Mnawajua, wako miongoni mwenu.
ReplyDeletehawa jamaa nao wakikamatwa wamwagiwe tindikali halafu waachwe na wala wasitibiwe.
ReplyDeletemaana mkiwafunga watakula ugali wa bure tu hawa.
Bwana David, binadamu wote ni sasa lakini nchi hazina power sawa. Hata sisi watanzania wakifanyiwa unyama Huko nje hatujakatazwa TBC, ITV na east Africa Kwenda kuchukua habari na kusambaza lakini tujiulize Swali vyombo vyetu vya habari vinaangaliwa na nchi ngapi? Kwa huo Mfano mdogo tu you can't compare the publicity.
ReplyDeletekwa asiekua na akili ndio anaunga mkono kitendo hicho@David V,Ugejua hao walikua ni volunteers,wanasaidia watoto wa ki Zanzibar na sio wazungu wenzao,unajua asilimia kubwa ya wazanzibar UK hata hawafanyi kazi wanatunzwa na tax za hao hao wazungu,ungejua hao wazungu ndio watalii maana we ukienda zanzibar hata kapu hununui!you should ZIP it,as terorism will never get you anywhere.
ReplyDeletemdau no 3 , si kweli binadamu wote ni sawa hii ipo kuwafurahisha wananchi tu wakati wa kuomba kura , lii uliona kiongozi wa serikali akajiweka kuwa sawa na raia? mfano mdogo tu nakupa tulifundishwa shule kila mtu ana haki ya kupewa heshima, lakini viongozi wetu wanataka zaidi , hawafurahi mpaka uwaite mhe...fulani , kwani ukiitwa kwa jina lako ulilopewa na wazazi wako ni tusi? basi usishangae raia wa majuu sio sawa na wewe na mimi ndugu yangu sisi tukiuliwa au kudhuriwa hata nyasi hazitikisi , lakini mwenzetu hata akipigwa kofi tu dunia nzima hutetemeka karibia kuanguka kwa sababu nchi zao zinawajali raia wao sio sisi viongozi wetu wameweka maslahi yao na familia zao mbele , wizi , rushwa na dhuluma dhidi ya raia.
ReplyDeleteHahaha wewe among Harpo juu punguza jazba hahah, no kweli inakera sana, Anony mwngine Harpo umesema kweli pia, Luna watz wanauwawa kinyama huko nje lakini cddhan kama serial I yet ilishawahi to a donge no no kwa ajili ya kubaidi halo wahalifu,,, binadadam wrote no sawa
ReplyDeletewatanzania wanauawa huko nje kwasababu ya biashara za madawa, bahati mbaya sana kama ilivyotokea DC.
ReplyDelete