Na Anna Nkinda- aliyekuwa Gaborone,  Botswana

Watanzania waishio nchi za nje wametakiwa kuwalea watoto wao katika misingi bora ya malezi yanayofuata mila, desturi  na utamaduni wa mtanzania ili waendane  na maadili ya kitanzania ya kuishi kwa unyenyekevu, upendo, ushirikiano na kuheshimu watu.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mke wa Rais  Mama Salma Kikwete wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na chama cha watanzania waishio nchini Botswana (ATB) katika hoteli ya Grand Palm mjini Gaborone nchini humo.

Mama Kikwete alisema kuwa ni vizuri watoto wawe na tabia njema inayokubalika na jamii ya kitanzania kuliko kulelewa katika mazingira yatakayowafanya wajue mila na tamaduni za nchi zingine kwani nyumbani ni nyumbani na ili  waendane na  hilo ni lazima walelewe kama  wazazi wao walivyolelewa.

“Ninawapongeza kwa  kuwa na umoja imara na wenye nguvu na ushirikiano ambao unawafanya kuwa kitu kimoja na pale ambapo jambo lolote linatokea liwe zuri au baya mnaweza kukabiliana nalo kwani  umoja ni nguvu na mahali penye upendo chuki hujitenga”, alisema Mama Kikwete.

Alisema ni jambo la kufurahisha kuona kuwa ndani ya  umoja huo kuna umoja wa kinamama ambao lengo lao ni  kuwaweka watoto pamoja na kuwafundisha mila na utamaduni wa mtanzania na kuwaomba wanawake ambao hawajajiunga na umoja huo waweze kujiunga  ili wajenge mshikamano ambao ni silaha kubwa ya watanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Tanzabia ilikuwa zamani, Enzi zetu, mitoto ya Tanzania ya siku hizi haina adabu hata kidogo, haiamkii, inamadharau, inajifanya kujua kumbe inaungua na jua, kazi kuvaa milegezo na kuiga marekani na western countries, unyenyekevu Enzi ya my hero- Mwalimu (RIP).

    ReplyDelete
  2. kila muda ukiendelea na mitoto inayokuja inakuja na adabu zao wakati wa mjerumani hapa bongo sisi tulikuwa na adabu kuliko mitoto iliyozaliwa wakati wa mwalimu(RIP) sasa hii mitoto ya kikwete haitofanana kitabia na mitoto ya rais wa chadema inayokuja.
    asante.
    mdau.
    iringa.

    ReplyDelete
  3. MILA NA DESTURI ZA KITANZANIA NI WIZI, ULAGHAI, RUSHWA, UKABAJI YAANI HAKUNA HATA MOJA CHA KUJIVUNIA.
    KILA MTU AMEKAA KIWIZI WIZI. HATA MTOTO AKIZALIWA LEO HOSPITALI BAHATI MBAYA NESI KAANGUSHA MKASI, MTOTO ATALIA MPAKA KICHA KINATAKA KUPASUKA. AKIULIZWA UNALIA NINI..."NESI KAOKOTA SHILINGI YANGU HALAFU KAIBANIA....!

    ReplyDelete
  4. Sio kila mila ya Tanzania ni nzuri.

    ReplyDelete
  5. Malezi ya watoto wako unamlaumu mzee Nyerere na mhe. Kikwete kweli? Wabongo tuache hizi, jilaumu mwenyewe kutoelimika kama mawazo yako finyu kiasi hiki, ukilea mtoto si balaa tupu

    ReplyDelete
  6. Sasa tuwalee watoto kwa mila na desturi za kitanzania and then how are they gonna fit in Ughaibuni culture? Ni sawa na kuwambia wageni walioko Tanzania wawalee watoto wao kwa mila za kwao. Sasa hapo TZ patakalika? Naona bora "do in Rome as the Romans do".

    ReplyDelete
  7. mimi naona ilikuwa ni ushauri na sio kuwaamrisha

    hata hivyo vijana wa Tanzania wameharibiwa sana na baba na mama zao hapa bongo..wizi, udanganyifu, utapeli, kujipatia kipato bila kufany akazi, uvivu, kutegemea kupewa, kufeli shuleni, kuvuta bangi, kusafirisha madawa ya kulevia, kubwia unga...ehe kweli wainge hayaaaa??

    kazi kwa washauriwa!

    ReplyDelete
  8. Mila za Kitanzania kumpiga mtoto ni jambo la kawaida. Lakini Ughaibuni ni kesi ya jinai na mtoto unanyanganywa. Ugahibuni uongo ni jambo la kawaida wa watu wazima.

    ReplyDelete
  9. Jamani wazazi tusitafute wa kumlaumu, tuanze sisi wenyewe kubadilika ili watoto wawe na mfano wa kuiga. Ikiwa Trafick anamwambia mwanae ngoja nirudi kutoka barabarani ntakuletea pocket money unategemea nini kwa mtoto huyu??

    Tuache tabia ya kulaumu watu, mtoto wako mwenyewe unataka umlaumu nani kama sio wewe mwenyewe na jamii inayokuzunguka ambayo inona mabadiliko ya mtoto wako na kuyafurahia. Au wakija kukwambia una ng'aka na kumtetea mwanao, then unategemea nani akurekebishie taifa la kesho????

    ReplyDelete
  10. Mfano mzazi anayeishi Darisalama,

    Asubuhi anawahi kazini, anasubiri daladala kituoni pembeni kuna mwanafunzi umri kama miaka mitano hivi,mkweche wa daladala unakuja, mzazi na yule mwanafunzi wanapigana vijembe na konda ili waingie mara konda anamvuta nje yule mtoto pwaa anadondoka.Mzazi aliyeingia na walioko ndani wooote kimya.

    Hitimisho hapo kuna tafsiri ipi ya malezi, yule mtoto anajifunza nini?

    ReplyDelete
  11. Mila za kitanzania ndio nini?? Nenda Dar sasa hivi ufanye tu utafiti kidogo. Utakuta baba ni Msukuma, mama ni Msukuma, watoto wanasoma english medium academy, hawajui kisukuma wala kiswahili. Mama anaweka nywele extension ziwe ndefu kama za wazungu ama za wahindi, watu maarufu kwenye jamii wanaweka nywele extension ziwe ndefu kama za wazungu, ...... sasa mila tunazoongelea hapa ni nini?

    ReplyDelete
  12. Wekeni dual citizenship hapo tutafurahia na kuwalea ki Tanzania pia.

    Hakuna jingine, sie hamtaki tuwekeze huko sasa watoto wetu wana passport za hizi nchi nyingine mnategemea tusipo walea kihuku itakuwaje nao inabidi tuwawekezee hapa hapa tulipo?

    Uraia wa nchi mbili mtatusikia kwa raha zote, kwa sasa mimi nasema nonono watajua maneno watakayoyajua na lugha yangu ya kikabila nyimbo wakumbuke milele wazazi walitoka wapi mbali na hilo. Wasahau watakuwa kama Obama kuendesha nchi za huku na kufanikiwa kimasomo in Jesus's name.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...