Kwaya ya uinjiisti kijitonyama kkkt ilifanya ziara ya kutembelea watoto yatima wa Kituo cha Kurasini Tarehe 11/08/2013, Kwaya hii imekuwa na utamaduni wa kuwatembelea watoto hawa kila mwaka ili kushiriki nao kuimba, kuwapa zawadi na kuwafundisha neno lamungu Kwaya ya Uinjilisti kijitonyama inaadhimisha miaka 25 (Jubilee) mwaka huu,mojawapo ya matukio kuelekea kilele cha Jubilee hii mnamo mwezi October 2013 ni kuwatembea watoto yatima na kuwapa msaada kutokana na mapato tuliopata kwa kuuza kazi zetu na michango toka kwa wanakwaya na ndugu jamaa na marafiki, pia tunatarajia kuzindua kanda ya dvd na cd mpya iitwayo Namtangaza Kristo mapema mwezi Septemba pia tuko katika hatua za mwisho za kuzindua studio ya kurekodia muziki iliyoko katika Jeengo la Kanisa kijitonyama pia kufanya tamasha kubwa la uimbaji litakaloshirikisha kwaya mbali mbali ikiwa ni pamoja na kwaya na waimbaji binafsi marafiki zetu hapa Dar Es Salaam na baadae mikoani na nje ya nchi, pia kwaya itatembelea sharika mbalimbali hapa dar es salam kwa ajili ya kutoa huduma ya uimbaji na kuitangaza album yetu mpya na zile za zamani, na mwisho kufanya ziara vijijini na kwenye missioni kwa ajili ya kupeleka Injili kwa njia ya |Uimbaji.

Hivyo tunawakaribisha washarika ndugu na jamaa kuwasiliana nasi katika maadhimisho haya kwa kutushauri lolote ili kulieneza neno la Mungu kwa njia ya Uimbaji

Kamati ya Habari Kwaya ya Uinjilisti Kijitonyama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...