Na Abdulaziz video, Kilwa
Wakaazi wa kijiji cha Kiranjeranje wilayani Kilwa, Mkoani Lindi, walifunga barabara kuu ya Kibiti-Lindi-Mtwara kwa kuweka magogo, na
mawe na kusababisha abiria na magari zaidi ya 50 kukaa kwa kipindi
cha masaa kadhaa kabla ya kutawanywa na kikosi cha kutuliza Ghasia,FFU.
Tukio hilo limetokea baada ya mwendesha bodaboda mkazi wa kijiji hicho
Bakari Magoyo (38) kugongwa na gari namba T489 AGA wakati alipokuwa
anavuka barabara hiyo.
Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wenzao waliokuwepo baada ya
kutawanywa kwenye tukio hilo,wakaazi hao walisema kuwa wameamua kufunga
barabara hiyo kwa kuweka mawe na magogo ili kuishinikiza serikali
kuweka matuta ya kupunguza mwendo kasi wa magari kwenye eneo la
makazi ya watu na ajali zinazotokea mfululizo katika eneo hilo.
,Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Lindi,George Mwakajinga amewataka wananchi kuacha tabia ya
kujichukulia sheria mikononi badala yake wafuate kanuni na taratibu
za kisheria.
Kamanda Mwakajinga alieleza kusikitishwa kwake na tukio la
kupigwa kwa dereva wa gari hilo, Omary Mkuwili, huku gari lake
likivunjwavunjwa na kuibiwa karibu vifaa vyote baada ya ajali hiyo.
Aidha alibainisha kuwa Mwendesha pikipiki aliegongwa alikimbizwa
hospitali ya mkoa ya Sokoine kwa ajili ya matibabu zaidi huku dereva
wa gari iliyogonga alipata majeraha makubwa baada ya kupata kipigo
na wananchi wenye hasira kali
Gari lililopata ajali kijijini Kiranjeranje, wilayani Kilwa
Nyinyi wananchi wacheni kupiga madereva bila ya kuangalia kosa ni la nani.
ReplyDeleteWaendesha bodaboda wengi hawazingatii sheria na hujivukia tu barabara au kuendesha kwa spidi kubwa kama sheria za barabara haziwahusu.
Hilo neno "Kijijiji" lina maanisha nini? Maana siku hizi kiswahili kina kua kwa kasi.
ReplyDeleteOhhh Majanga!
ReplyDeleteMdau Omari Mkuwili amenunua kiji Korola chake jijini Darisalama akasema acha niende nyumbani Kusini nikawasalimie anafika kijijini Kiranjeranje-Kilwa Wananchi wenye hasira kali wana mwangukia kwa maqkonde na magumi!
Kwa nini wanakijiji msingoje Trafiki apime kwanza ajali?