Askari Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiwa wamebeba sanduku lililohifadhi mwili wa Askari mwenzao, Marehemu Private Hugo Munga alifariki dunia Septemba 18 mwaka huu huko Pretoria Afrika Kusini kufuatia majeraha aliyoyapata akiwa na vikosi vya MONUSCO Congo DRC katika operations ya kuwaondoa waasi wa M23. Mwili wa Munga ulisafirishwa jana kwenda Mkoani Kilimanjaro kwa mazishi. Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa marehemu ilifanyika Viwanja vya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam.
Mama wa Marehemu, Jovitha Barnaba Munga akisaidiwa kuaga mwili wa mwanae.
Mkuu wa Majeshi, Jenerali Davis Mwamunyange akizungumza
Baadhi ya waombolezaji ambao ni Askari wenzake marehemu pamoja na wana familia wakiwa eneo la tukio.Picha Kwa hisani ya Father Kidevu Blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...