Mhe. Balozi Steven Matenje wa Malawi akiwa na Mhe. Palan Mulonda,Balozi wa Zambia nchini Marekani,(kulia) na Mhe. Martin Andjaba, Balozi wa Namibia nchini Marekani (kushoto)na Bw.Suleiman Saleh,Afisa wa Ubalozi wa Tanzania ,Washington DC katika hafla ya uzinduzi wa Malawi Washington Foundation iliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Mhe. Balozi Steve Matenje,Balozi wa Malawi nchini Marekani akimkaribisha Bw. Suleiman Saleh nyumbani kwake Potomac,Maryland katika hafla ya uzinduzi wa Malawi Washington Foundation mwishoni mwa wiki.
Mhe.Steve Matenje,Balozi wa Malawi nchini Marekani amesisitiza kwamba Tanzania na Malawi ni nchi ndugu na zenye historia kubwa baina ya wananchi wake na kubainisha kwamba tofauti katika suala la mpaka katika Ziwa Nyasa litamalizika si muda mrefu. Balozi Matenje aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa Washington Malawi Foundation iliyofanyika nyumbani kwake Potomac, Maryland.
Balozi alimweleza hayo Bw. Suleiman Saleh,Afisa Ubalozi wa Tanzania, Washington DC ambaye alimwakilisha Mhe.Balozi Liberata Mulamula katika uzinduzi huo.
Balozi Matenje aliendelea kusema kwamba anaamini udugu uliopo baina ya wananchi wa Malawi na Tanzania ndio unaompa imani kubwa kwamba suala la mpaka litapatiwa uvumbuzi wa kudumu na kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili.
Afadhali wewe Balozi wa ,Malawi MAREKANI Ambassador Steve Matenje angalau umetumia akili na busara zaidi ya Raisi wako Mama Joyce Banda!
ReplyDeleteKama ulivtyosema Uhusiano wetu ni wa kindugu na kuwa Suluhisho litapatikana hivi karibuni;
NI KUWA SULUHISHO TAYARI LIPO HAPO KAMA ALIVYO KUNUKU MICHUZI KATIKA MISTARI YA MWISHO YA CHINI...''Suala la Mpaka litapatiwa uvumbuzi wa kudumu na kwa manufaa ya wananchi wa nchi hizo mbili''...NI KUWA NINYI MALAWI MNA MAJI YENU KATIKA ZIWA(Sehenu yenu ya Ziwa) NA SISI TANZANIA TUNA MAJI YETU (Sehemu yetu ya Ziwa) HIVYO HILO NDIYO SULUHISHO LA KUDUMU!!!
Hivyo Malawi msihangaike kwenda Mahakama za juu huku mkiwa Masikini kwenu na msitarajie muujiza mwingine zaidi ya huu!!!
Mdau wa Kwanza umetumbua jipu!
ReplyDeleteNi muhimu Afisa Ubalozi wa Tanzania Ndugu Suleimab Saleh amifkishie ujumbe huu Balozi wa Malawi Marekani Steve Matenje.
Hivyo chezeni Rhumba kwenye Pati ya Malawi lakini watu wa Malawi wasitegemee msimamo wetu kibadilika kuhus Ziwa Nyasa, Rhumba likiisha kila mmoja akung'ute koti lake aende nyumbani kwake na Muhimu Mama Joyce BANDA afikishiwe taarifa hizi!!!