Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi. Jacqueline M. Maleko (pichani kulia) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).

Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo ulianza Septemba 10, mwaka huu, 2013.

Kabla ya uteuzi huu, Bi. Maleko alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Masoko, Wizara ya Viwanda na Biashara, kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade.
   
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.

DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera sana Jacqueline. Mungu akupe afya njema, hekima na busara katika jukumu hili. Stay blessed!

    ReplyDelete
  2. tunataka afanye kazi,sio tu tunasema stay blessed,atakuwa blessed kama atachapa kazi inavyotakiwa

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mama Maleko, kwa kazi nzuri unayofanya. Ubarikiwe na afya njema ili uweze kufanya kazi kwa bidii. Keep it Up dear.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...