Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bi.
Jacqueline M. Maleko (pichani kulia) kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TANTRADE).
Kulingana
na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi huo ulianza Septemba
10, mwaka huu, 2013.
Kabla
ya uteuzi huu, Bi. Maleko alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Masoko, Wizara
ya Viwanda na Biashara, kabla ya kuteuliwa kukaimu nafasi hiyo ya Mkurugenzi
Mkuu wa TanTrade.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
DAR
ES SALAAM.
Hongera sana Jacqueline. Mungu akupe afya njema, hekima na busara katika jukumu hili. Stay blessed!
ReplyDeletetunataka afanye kazi,sio tu tunasema stay blessed,atakuwa blessed kama atachapa kazi inavyotakiwa
ReplyDeleteHongera sana Mama Maleko, kwa kazi nzuri unayofanya. Ubarikiwe na afya njema ili uweze kufanya kazi kwa bidii. Keep it Up dear.
ReplyDelete