Zawadi ya T-Shirt ya Michuzi Blog 2014 itatolewa kwa washindi watatu wataotoa jibu sahihi ya ni jinsi gani tairi hili limewekwa hapo...Tuma majibu kupitia issamichuzi@gmail.com. Tarehe ya mwisho ni Oktoba 1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Hili tairi inawezekana limeunganishwa kwa moto sehemu ya juu ambayo hatuioni vizuri, baada ya kukatwa na kuwekwa kwenye mti huu kisha kuunganishwa tena, or inawezekana limekuwepo toka mti huu ni mchanga kabisa, lakini possibility ya pili ina utata maana ungeona hali ya kupauka kwa gurudumu baada ya kupigwa jua kwa muda mrefu toka mti ungali mchanga mpaka umefikia hapo, ni labda miaka minne au zaidi

    ReplyDelete
  2. Huo mti ulipokuwa bado mdogo hilo tairi lilitumika kuukinga usipate misukosuko kama kukanyagwa na wapiti njia n.k. hivyo ukaendelea kukua tairi likiwa hapohapo hadi leo

    ReplyDelete
  3. wakati mti ukiwa mdogo unakua ndipo tairi liliwekwa, kwahiyo umekua mpa umefikia hapo bado lipo, tairi haliozi litaendelea kuwepo

    ReplyDelete
  4. wakati mti ukiwa mdogo unakua ndipo tairi liliwekwa, kwahiyo umekua mpa umefikia hapo bado lipo, tairi haliozi litaendelea kuwepo

    ReplyDelete
  5. PHOTOSHOP image from Michuzi phot-studio Ltd

    ReplyDelete
  6. hilo taili limepakwa rangi nyeusi kutoa uchakavu wa jua,au ni kweli limeungwa huko pembeni baada ya kulivisha huwo mti,,,ama huwo mtu uliletwa hapo ukiwa tayali umeishakuwa mkubwa na ukavishwa hilo taili kupitia katika mizizi yake,
    Ahlam London

    ReplyDelete
  7. naenda kunywa kimpumu.

    ReplyDelete
  8. mdau wa kwanza hivi kweli unafikiri watu huku wana muda wa kupoteza kufanya hilo ulilosema? jambo la pili wewe umewahi kuchoma moto tairi au unabwabwaja tu?

    ReplyDelete
  9. hilo tairi limewekwa wakati mti bado mdogo... 0773564019

    ReplyDelete
  10. jibu rahisi sana, ivi wewe ukitaka kuvaa fulana una fanya vipi? huo mti matawi yake yalikunjwa pamoja halafu hilo tairi likavishwa juu, kama vile mtu akivua chuppi bila ya kuvua suruali.

    ReplyDelete
  11. Mie kwa fikra zangu, nadhani hilo tairi limekatwa likavishiwa kwenye hilo shina la huo mti, then ule upande uliokatwa ndio umefichika na hilo shina la mti kwa nyuma, tunaona shina kwa mbele upande uliaokatwa umekingika kwa nyuma, hivyo inapelekea kuonekana kama tairi hilo limeingizwa ima mti ulipokuwa mdogo au baada ya kupunguzwa matawi yote, wakati huenda ikawa hivyo sivyo kabisa.

    ReplyDelete
  12. toa jibu kupitia anuani pepe ya hapo kwenye tangazo,wote mlioandika majibu mmekosea kujibu hapa.
    Hili tairi ni uthibitisho tosa wa uchafuzi wa mazingiza,maana haliozi toka lilipowekwa wakati mti bado mdogo hadi sasa,na litaendelea kuwepo

    ReplyDelete
  13. Kwenye tairi mimi simo, ila munaojibu zingatieni vigezo na masharti hiyo T-shirt inaweza kuja Pemba halafu mukaishia kusema tumeroga.

    ReplyDelete
  14. Nakupa mji, Mtwara.

    ReplyDelete
  15. KWANI HILO NI TAIRI AU GURUDUMU?Ukijibu swali langu Michuzi na mm ndo nitajibu la kwako.

    ReplyDelete
  16. Tairi limewekwa wakati mti ulipokuwa mdogo,mti umeendelea kukua tairi likiwepo

    ReplyDelete
  17. Akili zangu kibongobongo hilo Tairi watu pia wangeshabeba labda limekatwa hapo kwa mshona viatu wa kienyeji kalishona na waya uwapande wapili huko! Mie naona mwenye jibu atatokea sehemu hizi Mwanza,au Tanga,au Pemba wakijibu hawa watu wataanza oh wameloga tehteh! MZ

    ReplyDelete
  18. Tairi liliwekwa wakati mti uanoteshwa.

    ReplyDelete
  19. Hilo tairi halipo kamili limekatwa halafu likavishwa katika huo mti na hiyo sehemu iliokatwa ni hiyo sehemu iliojizinga na Camera:) USA.

    ReplyDelete
  20. mti umezaa tairi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...