Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana amewataka mawaziri husika kutatua kero za wananchi baada ya watendaji wa chini kushindwa kufanya kazi zao, alisema sasa baadhi ya watendaji wamegeuza kero za wananchi mitaji na kuwachajisha pesa nyingi hasa wafugaji.
Akihutubia wakazi wa kata ya Mwasengela alisema mawaziri lazima wachukue jukumu la moja kwa moja kutatua matatizo ya wananchi, alisema wafugaji wa kata ya Mwasengela wamekuwa wakibughudhiwa na watu wa hifadhi ya Maswa kupita kiasi, alisema sheria zingine ziangalia wakati zinaweza zikawa zimepitwa na wakati hivyo ni vyema zikarekebishwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahaman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Mwangesela wilayani Meatu mkoani Simiyu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wakazi wa kata ya
Mwandoya ,kijiji cha Mandoya tarafa ya Kisesa ambapo Katibu Mkuu alipata
maelezo ya utekelezaji wa ilani ya CCM.
Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina akiwatambulisha wazazi wake kwenye mkutano wa hadhara ambapo aliwaambia wananchi ilimchukua miezi mitatu kukubaliwa kwa ombi lake la kutaka kugombea ubunge jimboni kwake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa kwenye picha ya pamoja na Mbunge wa Kisesa Ndugu Luhaga Mpina pamoja na wazazi wa mbunge huyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...