Na Mashaka Mhando, Handeni
KIWANDA kikubwa cha malighafi za kutengenezea Gilisi, Penseli na mitungi ya kuzimia moto (Fire Extinguisher ) kinajengwa katika kijiji cha Mkalamo kilichopo kata ya Kwamsisi wilayani Handeni, kinatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka ujao.
Mmoja ya wamiliki wa kiwanda hicho kijulikanacho kwa jina la Sino Tan ambacho kitatumia madini ya Glafiet , Bw. Mussa Mhezi anayeshirikiana na wachina, alisema taratibu zote za kijiji, kata na wilaya wamefuata ikiwemo kupata leseni ya kuchimba madini hayo.
Bw Mhezi alikuwa akimweleza Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dkt Abdallah Kigoda aliyetembelea kukagua kuanza kwa ujenzi wa kiwanda hicho, alisema kuwa wanatarajia kukamilisha majengo na kufunga mitano kabla ya Januari mwakani.
Alisema awali walikuwa wakichimba madini hayo na kuyapeleka nchini China lakini sasa ameamua kushirikiana na baadhi ya Wachina hao ambao watasaga madini hayo kisha kutengeneza malighafi hizo ambazo watauza hapa nchini kisha mengine kuyasafiorisha nje ya nchi.
"Hadi kiwanda kikianza kazi tunatarajia kuajiri watu 50 na tutakuw ana vibarua 100, mimi ni mzawa wa Handeni nimeonelea kiwanda hiki kijengwe huku kwetu ili kusaidia tatiuzo la ajira kwa vijana wetu na kuongeza uchumi wa wilaya na nchi," alisema.
Dkt Kigoda ambaye alifurahishwa na ujenzi wa kiwanda hicho, kutokana na kwamba itasaidia wananchi kupata ajira, kuongeza uchumi wa wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla hatua ambayo aliwapongeza na kuaahidi wizara yake kuwapa ushirikiano ili kukamilisha hatua hizo za ujenzi.
Hata hivyo, aliwataka wafike Wizarani kwake kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine za kiserikali ili waweze kuendelea na ujenzi huo ambao unafanyika katika eneo hilo licha ya wananchi kupata ajira pia watanufaika na nishati ya umeme itakayofika kiwandani hapo.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko Dkt Abdallah Kigoda (kwanza Shoto) akikagua ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha malighafi ya kutengeneza Gilisi kinachojengwa katika kijiji cha Mkalamo wilaya Handeni kinachoitwa Sino Tan limited, kushoto kwa waziri ni mmoja ya wakurugenzi Bw. Mussa Mhezi.
Waziri Kigoda na baadhi ya wananchi wakitazama msingi wa kiwanda hicho ambacho kimeelezwa kwamba kitakuwa ukombozi mkubwa kwa wananchi.
Dkt Kigoda akizungumza na wananchi wa mji wa Kabuku nje kuhusiana na mambo mbalimbali akiwemo ujenzi huo wa kiwanda.
Bw Mussa Mhezi aliyeshika kipaza sauti akiwa na Wachina ambao wanajenga kwa pamoja kiwanda hicho.
Gilisi ni kitu gani wadau?
ReplyDeleteMwulize Dr. Kigoda wa handeni.
ReplyDeleteNaomba kuelimishwa jamani. Gilisi ni nini?
ReplyDelete