Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea hati ya uraia wa hiari wa Jimbo la Nebraska nchini Marekani iliyotolewa na Secretary of State wa Jimbo hilo Bwana John Gale. Anayekabidhi hati hiyo kwa Mama Salma ni Dkt. Marjorie Kastelnik, Dean, College of Education and Human sciences wa Chuo Kikuu cha Nebraska nchini Marekani tarehe 28.9.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, (WAMA), Mama Salma Kikwete akitoa keynote address kwenye' workshop on Viewing English Education through a Globalized Lens' iliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Nebraska huko nchini Marekani tarehe 28.9.2013.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Dr. Dzingai Mutumbuka, Chairman of the Association for the Development of Education in Afrika and Former Minister of Education in Zimbabwe mara baada ya Mama Salma kuhutubia mkutano Global Education huko Nebraska nchini Marekani tarehe 28.9.2013.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Mke wa Gavana wa Jimbo la Nebraska Mama Sally Ganem. 
Mke wa Gavana wa Jimbo la Nebraska Mama Sally Ganem akifanya mazungumzo na mgeni wake Mama Salma Kikwete alieambatana na Balozi wa Tanzania Nchini Marekani,Mh. Liberata Mulamula.
Mke wa Gavana wa Jimbo la Nebraska Mama Sally Ganem akiagana na mgeni wake Mama Salma Kikwete.PICHA NA JOHN LUKUWI.


UKOSEFU WA ELIMU UNAWAFANYA WATOTO KUKABILIWA NA TATIZO LA UJINGA, MARADHI NA UMASKINI - MAMA SALMA  KIKWETE

Na Anna Nkinda, Lincoln
Watoto wengi  katika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na tatizo la ujinga, maradhi na umaskini hivyo basi kupatikana kwa elimu bora kutawasaidia kujikwamua na matatizo hayo pindi watakapomaliza masomo yao na kupata ajira na hivyo  kujikwamua na hali ngumu ya maisha.
Hayo yamesemwa jana na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete wakati akiongea na walimu walioshiriki katika warsha ya elimu iliyoandaliwa na Taasisi ya Malaika na kufanyika katika chuo kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln .
Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) alisema jamii nyingi inajitahidi kupambana na matatizo yanayozakabili  watoto wao  lakini kama kutakuwa na ushirikiano wa pamoja itasaidia matatizo hayo kutatulika kirahisi.
“Warsha hii inaonyesha kuwa Dunia ni moja, ni kama kijiji bila ya kuangalia mipaka iliyopo , kutokana na hili tunatakiwa kutumia utaalamu wetu katika kushirikiana kwa pamoja ili kutatua matatizo yanayotukabili na kutumia pamoja rasilimali zilizopo”, alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya Malaika Dk. Natalie Hahn alimshukuru Mama Kikwete kwa kukubali kushiriki katika warsha hiyo kwa kuwa ni wanawake wachache kama yeye wanaoweza kuwa karibu na jamii inayowazunguka.
Alisema kuwa elimu ni nyenzo  muhimu katika maisha mtu akiwa na elimu anaweza  kwenda popote pale apatakapo kutokana na hilo ndiyo maana anachangisha vitabu kwa ajili ya wanafunzi katika mabara yote ili nao waweze kupata elimu kama aliyoipata yeye.
“Walimu mnatakiwa kuwa wa kimataifa ili muweze  kufundisha na wengine wajivune na kutaka kuwa kama nyinyi, mtafute wafadhili wa masomo yenu ili muweze kusoma zaidi pia muwasaidie watoto ambao wanahitaji kusaidiwa kwani kama mtoto akikosa ada au nguo za shule Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshugulikia watoto (UNICEF) linawasaidia watoto wa aina hii”, alisema Dk. Natalie.
Aliwataka walimu walioshiriki katika kongamano hilo wajitahidi kuwa na shule dada nchini Tanzania na kujenga mahusiano nao ili waende kufundisha kule watajifunza mambo ambayo ni tofauti, watumie rasilimali walizonazo kuwasaidia wanafunzi ili nao wawakufundishe wengine.
Katika warsha hiyo  Mama Kikwete alikabidhiwa  hati ya ukazi wa jimbo la Nebrasca na Dk. Marjorie Kastelnin ambaye ni mlezi wa wanafunzi katika kitivo cha Elimu na Sayansi ya Jamii.
Mama Kikwete pia alikutana na Mke wa Gavana wa jimbo hilo Mama Sally Ganem ambaye alimpongeza kwa kazi kubwa anayoifanya nchini Tanzania ya kuwasaidia kina mama na watoto wa kike kupata elimu.
“Kazi unayoifanya ni kubwa kwani inagusa maisha ya watu, elimu ni kitu cha muhimu sana katika maisha ya binadamu mtu bila ya kuwa na elimu hawezi kufanya kitu chochote wewe unawasaidia watoto wa kike kupata elimu na kuwaandalia maisha yao ya baadaye, nakupongeza sana kwa hilo”, alisema Mama Ganem.
Alisema kuwa fani yake yeye ni mwalimu kutokana na majukumu aliyonayo hafundishi kwa sasa, lakini  kwa kuwa anawapenda watoto ameanzisha program ya kutoa chakula cha asubuhi kwa wanafunzi wa shule za msingi jambo ambalo mme wake Gavana Dave Heineman amemuunga mkono kwa kutoa chakula cha mchana kwa watoto hao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera mama Kikwete.
    Huyu mama anajua kuvaa. Kweli anaiwakilisha Tanzania vilivyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...