Ankal akipongezwa na blogger gwiji duniani kaka Ndesanjo Machas iku alipoanzisha rasmi Globu ya Jamii katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki, Finland, Septemba 8, 2005 (BOFYA HAPA)
 Ankal na mai waifu wake na toto tundu Sellah wakikata keki kuadhimisha miaka 9 ya Globu ya Jamii usiku huu
Ankal na familia yake wakisherehekea kimya kimya hepi besdei ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii usiku huu.
-----------------------------------------------------------
Ilikuwa siku ya Alhamisi tarehe kama ya leo (Septemba 8,) miaka TISA iliyopita wakati Globu ya Jamii ilipozaliwa rasmi katika ukumbi wa mikutano wa Finlandia jijini Helsinki Finland, kama utani tu. Kwa msemo mwingine, ni miaka TISA kamili leo toka Globu ya Jamii ianze Libeneke la kuhabarisha wadau kwa mapicha na habari kemkem bila kukosa hata siku moja
Kikosi kazi cha Globu ya Jamii kingependa kutoa shukrani za dhati kwa wadau wote duniani kote kwa kampani mnayotupa kila saa, siku, wiki, miezi na hadi sasa ikiwa ni MIAKA TISA kamili.  Si jambo dogo, ukizingatia katika safari hii njiani tumekutana na kila aina ya changamoto, kubwa kuliko yote ikiwa ni kufanya kila tuwezalo kubakia hapa tulipo kwa kufuata weledi pamoja na sera ya HATUBAGUI, HATUCHAGUI; ATAYETUZIKA HATUMJUI, pamoja na kauli mbiu kwa wadau watoa maoni ya kuwa waangalifu kutochafua hali ya hewa wala kujeruhi hisia ya mtu wakati wa kutoa maoni.
Si rahisi kumridhisha kila mdau, na kwa mujibu wa usemi wa Kimombo wa “What’s good for the goose is bad for the hen” unaomaanisha hivyo. Yaani “Kilicho kizuri kwa bata mzinga, ni kibaya kwa kuku”.
Katika kuadhimisha hii MIAKA TISA ya Libeneke, Globu ya Jamii haitofanya sherehe ya pamoja na wadau kama ilivyotarajiwa. Badala yake Ankal kajikakamua na kununua kajikeki na kukata na kula na familia kwa niaba ya wadau. Ila ahadi yetu ni kwamba, panapo majaaliwa, sherehe kubwa itaandaliwa mwakani wakati wa kuadhimisha MIAKA KUMI. Ni mapema mno kusema itakuwaje, ila panapo uhai itakuwa  SHEREHE KUBWA na inayostahili.
Kwanza kabisa tunamshukuru Jalali Muumba wa vyote kwa tunu hii aliyoitupa. Tunatambua kuwa tuna bahati ya sisi kuwa sisi, na kamwe bahati hiyo uliyotupa, EWE MOLA, hatutoichezea...
Globu ya Jamii pia inachukua nafasi hii kuwashukuru wadhamini wake, ikiwa ni pamoja na VODACOM, AIRTEL, UHURU ONE,  TTCL, NMB, NBC, AZANIA BANK, CRDB, NHC, PRECISION AIR, AIR UGANDA, NSSF, PSPF, DSTV, SKYLINK, SERENGETI FREIGHT FORWADERS  ‘WAZEE WA KAZI’, SWIFT FREIGHT, GIRAFFE OCEAN VIW HOTEL, DR MKOMBOZI,  na wengineo wote. Tunashukuru kwa kutuamini na kuendelea kuendeleza nasi Libeneke. 
Shukrani zingine  za kipekee ziende kwa familia yangu kwa uvumilivu wanaoonesha kwangu, pia kwa wadau kadhaa ambao tukiamua kuwataja wote hapa itachukua ukurasa wote hu na tusiwe tumetaja japo robo yao. Kwa uchache tu, na ambao ni kwa niaba ya wale ambao hatutotaja kwa ufinyu wa nafasi na pia si  kwa ubora wao, shukrani hizo zimwendee kaka Ndesanjo Macha kwa kuwa wa kwanza kutufungulia na kutuongoza njia na kutupa maudhui ambao baada ya kuyafuata, tumeona faida yake.
Washauri wakuu wetu pia hatuwasahau katika hili. Nao  ni Profesa Mark Mwandosya, Mhe. January Makamba, Freddy Macha, Balozi Peter Kallaghe, Othman Michuzi, Ahmad Michuzi, Christopher Makwaia MK, Steve Wassira jnr., Nathan Chiume, DJ Luke Joe wa Vijimambo, Waziri Ally, John Kitime, Alex Perullo, Muhidin Maalim Gurumo, kaka Jeff Msangi, Boniface Makene, Kirk Gills, Oscar Shelukindo, Ephraim Mafuru, Imani Kajula, Profesa Mbele, Da' Chemi Chemponda, Ankal Beda Msimbe, kaka Assah Mwambene, Da' Tagie Daisy Mwakawago, Shamim Zeze wa 8020 Fashions, Mama wa Mitindo Asia Idarous na mumewe Mzee Khamsin, Ainde, kaka Asimwe Kabuga, Abdallah Ezza na Fide Tungaraza wa Heslsinki na wengineo wengi tu. Ushauri wenu tunauthamini na kuuheshimu!
Wengine ni viongozi wote wakuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Spika, Naibu Spika na maofisa wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waheshimiwa Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano pamoja na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Viongozi  maofisa wote wa vyama vya siasa, Viongozi wote na watumishi  wa taasisi za umma na binafsi, Mablogger wote na mwisho ni wadau wote wanaotupa moyo kila kukicha. Asanteni sana, sana,  sana, sana. Hatuna cha kuwapa zaidi ya hizo SHUKURANI kutoka katika kilindi cha moyo wetu. MOLA AWE NANYI, NA AWAZIDISHIE PALE PALIPOPUNGUA.
Hatuna la zaidi la kusema zaidi ya kuahidi kwamba tutaendeleza Libeneke kwa moyo wetu wote huku tukipiga magoti kuwaomba wapendwa wadau wetu duniani kote muendelee kutupa kampani, kwani bila ninyi sisi si lolote si chochote. Pia tunaomba radhi pale tunapoteleza kama binaadamu yeyote ambaye daima duni si mkamilifu, ambapo likitokea litalotokea si kwa makusudi ama nia mbaya bali ni kwa udhaifu huo huo wa kibinaadamu.

Naomba kuwasilisha,
Wenu Mnyenyekevu,
Muhidin Issa Michuzi “Ankal”







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Wow!!! Wow!!! Wow!!! Congratulations! Beautiful family indeed. You are very blessed uncle.Thank you for keeping us informed on a whole host of news. Keep up the good works!

    ReplyDelete
  2. Bwana Michuzi, kama blogu uliianzisha Septemba 8, 2005 basi bado haijafikisha umri wa miaka 9. Ni miaka minane (8) ndiyo imefikisha.

    ReplyDelete
  3. fundi kombo ramadhaniSeptember 08, 2013

    HONGERA SANA KAKA, TUTAENDELEA KUFUATA NYAYO ZAKO.

    ASANTE
    FUNDI KOMBO

    ReplyDelete
  4. HONGERA BRAZA NA FAMILIA YOTE!
    MOLA AWABARIKI NA AWAZIDISHIE KILA KITU!
    AMINA!
    TOKA: www.sokainbongo.com

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Ankal Muhidin Issa mIchuzi, ulianzaisha njia nzuri na sasa kuna wengi kwenye Tasnia hii ila wewe hujababaika nakuamua kusimamia msimamo wako na maadili kwani ni Blog yako pekee ndio inayokidhi mahitaji ya watu wa marika yote, na pia haiendekezi mambo ya uchafuzi wa maadili. mwenyezi Mungu ajaalie Mwakani tufike salama tuadhimishe miaka kumi In Sha Allah. Mwenyezi Mungu akubariki Afya njema wewe na wana MMG.

    ReplyDelete
  6. Congrats on your 9th Anniversary..Keep the blog going..we need you..

    ReplyDelete
  7. HONGERA KAKA MICHUZI KWELI SAFARI NI HATUA
    MDAU

    ReplyDelete
  8. TUNAIOMBEA KILA LA HERI BLOGU YA JAMII,KATIKA KUSHEREKEA MIAKA 9 YA KUZALIWA,MIAKA 9 KATIKA LIBENEKE,
    SIO MCHEZO ! UKURUGENZI WAGLOBU YA JAMII NA TIMU YAKE UMEFANYA MENGI
    MAZURI NA KULETA MAPINDUZI YA HABARI
    NA MAENDELEO.
    MUNGU IBARIKI BLOGU YA JAMII
    ina libeneke lake

    Wadau Ngoma Africa Band aka FFU Ughaibuni

    ReplyDelete
  9. Duh harafu FFU Ngoma Afrika na kamanda wao naona hawakutupi mtoto wa kariakoo mwenzao

    ReplyDelete
  10. Hongera saana anko Michuzi mwendo ulikuwa mrefu lakini sisi wadau tumepata mafanikio mema,bloggi ya jamii imewafungulia njia wana-bloggi chipukizi wengi kujifunza toka kwako binafsi na hata kutoka bloggi ya jamii kwa jamii.
    Kila la kheri pamoja na familia.

    mdau mikidadi
    denmark

    ReplyDelete
  11. Congrats na Mungu akuzidishie.
    Hiyo methali yako ya kimombo imenifurahisha sana maana hii ni awal mara kusikia methali hiyo hivyo.
    Eat and drink your fill, but you always remember the Provider.
    Mabrook mara elf
    ibrahim

    ReplyDelete
  12. Hongera kwa MIAKA 8 na sio tisa Ankal.

    ReplyDelete
  13. Blogu imeanzishwa Septemba 8, 2005. Iweje iwe imefikisha miaka 9? Ni miaka 8. Ni vyema ungerekebisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...