Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe na kufungua pazia katika jiwe la msingi ikiwa ni ishara ya Ufunguzi rasmi wa Jengo la Madarasa ya Shule ya awali ya Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini.ambapo baadae aliendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi ya Kanisa hilo ambapo zaidi ya shilingi Milioni 212 zilipatikana zikiwemo na ahadi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipanda Mti katika eneo la Kanisa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwapungia mkono waumini wa Kanisa la AICT (Africa Inland Church Tanzania) Pastoreti ya Kahama Mjini,wakati alipokuwa akiwasili kwenye kanisa hilo kwa ajili ya kuendesha Harambee ya Kuchangia Ujenzi wa Shule ya Msingi wa ya Kanisa hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...