Msanii
wa muziki wa kizazi kipya Mwansiti Almasi,akifafanua namna
anavyonufaika na huduma za NSSF,mara tu walipojiunga kupitia kundi lao
la Lekadutigite,ndani ya semina ya fursa twendzetu iliyofanyika ndani ya
ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi.
Mbunifu
wa mavazi kutoka mkoani Morogoro,ambaye pia ni mjasiliamali
aliyejitambulisha kwa jina la Diana Magessa akionesha mbele ya washiriki
wa semina ya Fursa kwa Vijana (hawapo pichani) baadhi nguo zake
alizozidizaini kwa ubunifu wake.
Meneja huduma wa Wajasiliamali-Zantel akizungumza mbele ya sehemu ya wakazi wa Morogoro waliojitokeza kwenye semina ya Kamata fursa twendzetu,kuhusiana na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya kampuni hiyo,Semina hiyo iliofanyika ndani ya
ukumbi wa Katema Hall,Midland hotel mkoani Morogoro mapema leo asubuhi iliwakutanisha wadau mbalimbali.Semina ya kamata fursa twendzetu inaratabiwa na Clouds Media
Group,ambapo kwa sasa imekwishafanyika ndani ya mikoa zaidi ya
nane,ikiwemo Kigoma,Singida,Tabora,Dodoma,Mtwara,Mbeya,Morogoro pamoja na Iringa.

Mkurugenzi wa Vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba akifunga semina ya kamata Fursa twendzetu kwa vijana, iliyofanyika mapema leo mkoani Morogoro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...