Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
TAARIFA
KWA UMMA
Wizara
ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Uongozi wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa
pamoja na wadau wa tasnia ya utalii nchini wanayo furaha kuwakaribisha wananchi
wote na wadau mbalimbali katika maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani kwa mwaka
2013 ambayo Kitaifa yatafanyika Mkoa wa Mwanza.
Siku
ya Utalii Duniani huadhimishwa tarehe 27 Septemba ya kila mwaka ambapo kila
nchi mwanachama wa Shirika la Utalii Duniani husheherekea siku hii. Kwa mwaka
huu Kimataifa, maadhimisho haya yatafanyika katika Visiwa vya Maldives.
Kauli
mbiu ya mwaka huu ni “Utalii na Maji –
Kulinda Hatma Yetu (Tourism and Water – Protecting Our Common Future)”. Kwa
kuzingatia kauli mbiu hii, tunawajulisha wadau wote katika nyanja mbalimbali za
uhifadhi mazingira, matumizi ya teknolojia sanifu, wafanyabiashara wa tasnia ya
utalii na maliasili, wadau wa sekta ya maji, taasisi za elimu, wanasiasa,
viongozi na wataalamu mbalimbali kushiriki katika wiki ya maadhimisho ya utalii
duniani.
Shughuli
zitakazofanyika ni pamoja na tafsiri ya kauli mbiu katika Nyanja mbalimbali
kama, mashindano ya uandishi wa insha mbalimbali kuhusiana na mada, michezo na
burudani mbalimbali, maonesho ya utalii, malikale, misitu na masuala ya uhifadhi
kwa ujumla, teknolojia mbalimbali,
pamoja na ziara ya kutembelea Hifadhi ya Saanane.
Wananchi
pamoja na wadau wote mnakaribishwa sana kushiriki katika maadhimisho haya.
“Kumbuka Utalii ni nyenzo ya kuhamasisha uhifadhi kwa
uhai na ustawi wa Taifa”
Imetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Maliasili
na Utalii,
S.L.P 9372,
DAR ES SALAAM.
Simu: 255-22-2864230
Barua pepe: ps@mnrt.go.tz
Tovuti: www.mnrt.go.tz
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...