Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akitia saini kitabu cha maombolezi katika ubalozi wa Kenya nchini Tanzania kufuatia mashambulizi ya Kigaidi nchini Kenya yaliyotokea hivi karibuni.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Kaimu Balozi wa Kenya nchini Tanzania George Awenour baada ya kutia saini kitabu cha maombolezi.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif akiangalia bidhaa mbali mbali katika maonyesho ya India yaliyofanyika viwanja vya sabasaba Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Biashara na Viwanda wa India Dr. D. Purandeswari, akitoa maelezo kuhusiana na maonyesho ya biashara ya India yanayofanyika viwanja vya saba saba Dar es Salaam.
Kiongozi wa ujumbe wa wafanyabiashara wa India Sanjay Kirloskar, akimkabidhi zawadi Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad katika maonyesho ya biashara ya India yanayofanyika viwanja vya saba saba Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akihututubia katika ufunguzi wa maonyesho ya biashara ya India katika viwanja vya saba saba Dar es Salaam.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na viongozi mbali mbali wakiingia katika ukumbi wa mikutano katika viwanja vya saba saba Dar es Salaam. Picha na Hassan Kombo


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...