Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akishirikiana na
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa kukagua vifaa vya
michezo muda mfupi kabla ya Waziri kukabidhiwa rasmi vifaa hivyo
vitakavyotumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es salaam.
Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim.
Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala akipokea vifaa vya
michezo kutoka kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa.
Vifaa hivyo vitatumika kwenye mashindano maalum ya Sekondari Mkoa wa Dar es
salaam. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim. Vodacom
ilikabidhi jezi za soka seti 12, mipira 40 na kombe kubwa la Mshindi
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Dk. Fenella Mukangala akipokea kombe kubwa kutoka kwa Mkuu wa Masoko na
Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa atakalokabidhiwa mshindi wa kwanza wa
mashindano maalum kwa shule za sekondari Mkoa wa Dar es salaam yanayoandaliwa
na Wizara.Kushoto ni Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo Juliana Yasoda. Vodacom ilikabidhi
pia jezi za soka seti 12 na mipira.
---------------------------
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangala leo amepokea
vifaa vya michezo kutoka Vodacom kwa ajili ya kutumika kwenye mashindano maalum
ya sekondari yanayotarajiwa kufanyika mwezi ujao jijini Dar es salaam.
Akipokea
vifaa hivyo ambavyo ni jezi seti 12 na mipira 40 pamoja na kombe kwa ajili ya
bingwa wa michuano hiyo Waziri Dk Mukangala ameelezea kufurahishwa kwake jinsi
ambavyo Vodacom walivyopokea ombi la Wizara la kusaidia mashindano hayo.
Amesema
lengo la mashindano hayo ni kuendeleza azima ya serikali ya kutengeneza fursa
ya ukuzaji na uendelezaji michezo kwa ngazi za chini kupitia falsafa ya michezo
jamii.
“Michezo
ni gharama inahitaji fedha nyingi kugharamia vifaa, mafunzo kwa walimu, viwanja
na gharama nyengine za uendeshaji ndio maana naipongeza sana Vodacom kwa
kukubali ombi letu la kusaidia mashindano haya maalum yatakoyoshirikisha shule
12 za sekondari za Mkoa wa Dar es salaam.”Alisema
“Mashindano
haya ni ya majaribio tukiangalia namna ambavyo tunaweza kuwekeza vya kutosha
kwenye michezo ngazi ya mashuleni kwa nchi nzima, tutaanza na mchezo wa soka
ila mipango ni kupanua wigo kwa kuongeza mpira wa pete na riadha kwa hapo mwakani
ikihusiha mikoa mingi zaidi.”Alisema Dk. Mukangala
Waziri
Dk. Mukangala amesema Wizara yake inaimani kubwa juu ya mpango huo huku
akizitaka jamii kuyapokea na kuyaona kuwa ni sehemu yao ili pamoja na kuyapapa
mafanikio bali pia kuwatia moyo watoto wakati wote watakapokuwa waskishiriki.
Amesema
kuwa anatambua kuwa mahitaji ni makubwa na kwamba kila shule hapa nchini
ingependa kushiriki lakini kwa kuanzia watachagua shule 12 za sekondari kama
majaribio huku mipango ikiendelea kuwekwa sawa ili mashindano hayo yawe mapana
zaidi kwa hapo mwakani.
“Tuna
shule nyingi hapa tu Dar es salaam tumepata wakati mgumu sana kuchagua
wawakilishi wa kila Wilaya lakini kwa sasa tunaanza na hizo chache tukiwa na
Vodacom na baada ya kumalizika tutafanya tathmini kuona namna ya kuyaongezea
wigo wa ushiriki na wa kijiografia.”Alisema Dk. Mukangala
Kwa
upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa
amesema Vodacom inatambua umuhimu wa kuwaandaa wachezaji katika ngazi za chini
ili kuwa na uhakika wa maendeleo ya michezo nchini.
“Kukubali
kwetu kuwa wadhamini kumesukumwa na imani yetu juu ya maendeleo ya michezo
nchini tukiamini katika kuwekeza kwa wanafunzi mashuleni, leo tunafuraha kuwa
sehemu ya miapngo ya serikali kukamilisha kile ambacho kila mtu anapenda
kukiona kikifanyika katika michezo.”Alisema Twissa
“Tumekuwa
wadhamini wa Ligi Kuu Vodacom ambayo imekuwa ikipiga hatua kubwa kimaendeleo
hasa kwenye eneo la ushindani hivyo ili mafanikio hayo yawe endelevu ni lazima
tuwe na misngi mzuri wa kuzalisha wachezaji wenye ubora na viwango na kwamba njia
moja ya msingi ni kuwa na mashindano ya ngazi za chini hasa mashuleni”Alisema
Twissa
Amesema
vifaa walivyovitoa ni sehemu ya Vodacom kuunga mkono juhudi za serikali za
kutekeleza mikakati ya uzalishaji, ukuzaji na uendelezaji wa vipaji na kwamba
Vodacom inafurahia mpango huo.
Mashindno
hayo maalum yataratibiwa na Baraza la Michezo la Taifa – BMT na kwamba
utaratibu umewekwa wa kuapat sekondari 12 kutoka Wilaya tatu za Mkoa wa Dar es
salaam ambapo kila Wilaya itatoa sekondari
4.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...