Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa wito kwa waislamu kuungana kutokana na mambo ya msingi yaliyomo katika dini hiyo na kuacha kutofautia kwa sababu ya madhehebu.
Amesema kuwa na madhehebu tofauti ni neema katika dini, hivyo hakuna sababu ya kugawanyika kutokana na tofauti ya madhehbu waliyonayo waislamu.
Maalim Seif ametoa nasaha hizo wakati akifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa iliyofanyika Mjini Sumbawanga, Mkoani Rukwa.
Amesema ni jambo la kushangaza kuona waislamu wanakubaliana katika mambo ya msingi, lakini wanatofautiana na kulumbana kwa mambo madogo ambayo hayana athari ndani ya misingi na mihimili mikuu ya dini.
Amefahamisha kuwa iwapo waislamu wataungana na kuwa kitu kimoja, wataweza kuwashinda maadui wa Uislamu ambao siku zote wamekuwa wakishabikia migawanyiko ndani ya dini hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...