Fredrick Mwakalebela akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa timu zitakazoshiriki Mwakalebela Cup mara baada ya kuwakabidhi vifaa mbalimbali vya michezo.


Fredrick Mwakalebela akimkabidhi moja ya seti ya jezi kiongozi wa timu ya Upendo Fc Dudu Harun kwa ajili ya kushiriki ligi ya wilaya inayojulikana kama Mwakalebela Cup. Hafla iliyofanyika katika ukumbi wa New Ruaha International Lodge mwishoni mwa wiki(picha zote na Denis Mlowe).
==========  ======== ========
MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 MKOANI IRINGA

Na Denis Mlowe,Iringa

ALIYEKUWA Katibu wa TFF Fredirick Mwakalebela  amemwaga vifaa vya michezo kwa timu 13 zinazotarajia kushiriki ligi soka wilaya ya Iringa na timu za kike na kiume za wasanii wa filamu vyenye thamani ya shilingi milioni 11.

Mwakalebela amekabidhi vifaa hivyo vya michezo kwa viongozi wa timu shiriki ikiwemo mipira 5 kwa ajili ya ligi ya wilaya na mpira mmoja kwa kila timu shiriki, jezi seti moja kwa kila timu, filimbi, vibendera na shilingi milioni 3 za maandalizi ya ligi hiyo.

Timu zilizokabidhiwa vifaa hivyo ni Zimamoto na Uokoaji, Black Eagle fc, Mtwivila Fc, Mkimbizi Fc, Isakalilo Fc, Real Moja moja, Iringa City na Upendo,Don Bosco, Ruaha Shooting Mtwa Fc na Black Cheeter ambazo zinatarajia kushiriki ligi hiyo itakayojulikana kama Mwakalebela Cup. Timu za wasanii wa filamu Iringa Movie walijipatia jezi za soka kwa upande wa timu ya kiume na netiboli zilifaidika na msaada huo wa vifaa vya michezo baada ya kuwapatia ahadi ya vifaa miezi ya nyuma.

Mwakalebela  aliasema kuwa moja kati ya mambo ambayo yamekuwa yakikwamisha vijana kusonga mbele kimichezo ni kutokana na kutokuwepo kwa umahamasishaji wa kutosha kutoka kwa viongozi na wadau wengine ambao wanaweza  kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele kwa michezo ya vijana na kukuza soka katika mkoa wa Iringa.

Mwakalebela amewataka viongozi wa chama cha soka kuhakikisha  ligi hiyo iwe ya haki na kumpata bingwa wenye vigezo kwa lengo kuondoa lawama zisizo na msingi kama mashindano yaliyopita. “Naomba sana viongozi husika kuyasimamia vema mashindano haya nikiamini kuwa bingwa atapatikana kwa haki na  yatachangia sana katika kuinua ari ya michezo  kwa mkoa wa Iringa” alisema Mwakalebela.

Alisema baada ya miaka miwili tunahitaji kuwa na timu ya soka ambayo itakuwa inashiriki ligi kuu soka Tanzania bara hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuweza kuhakikisha soka linakuwa kwa mkoa wa Iringa.  Aidha alisema kwa ajili ya kuongeza ushindani zaidi katika mashindano hayo, mshindi wa kwanza katika katika ligi ya wilaya atazawadiwa shilingi laki 5 na kutakuwa na zawadi kwa mfungaji bora, mchezaji bora wa mashindano, kocha bora, na refa bora.

Mwakalebela aliomba chama cha soka mkoa wa Iringa kumwongezea udhamini wa mashindano hayo ikiwa ni msimu wa pili kuweza kudhamini mashindano haya yanayopendwa kwa kiasi kikubwa na mashabiki wa soka kutokana na upinzani uliopo kwa timu hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Sawa Kiongozi Mwakalebela,

    Umegawa Jezi za Yanga peke yake mbona sisi wa Msimbazi hapa Iringa umetutenga?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...