Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii Moshi.
WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi imesema imejipanga kukabiliana na
mashambulio ya kigaidi kama lile lililotokea hivi karibuni katika
jengo lenye maduka makubwa ya biashara la Westgate ambapo zaidi ya
watu 60 wameuawa huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya.
Tukio hilo la kihistoria lililotikisa Jiji la Nairobi nchini Kenya kwa
takribani siku nne limechangia pia kuwepo kwa hali ya tahadhari kwa
Tanzania na sasa hofu imetanda ndani ya mikoa iliyo jirani na Kenya na
hata katika maduka makubwa yanayo milikiwa na wakenya kama Nakumat
lililopo mjini Moshi.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa maofisa
wanadhimu,wahasibu na maofisa mipango wa mikoa na vikosi wa jeshi la
polisi ,naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Mwamini Malemi
alisema serikali iko tayari kukabiliana na hali yoyote ile ya kigaidi.
Alisema kutokana na tukio hilo la Kenya nchi imepata fundisho ya nini
kinatakiwa kufanyika kwa sasa katika kukabiliana na hali hiyo huku
akiwataka wananchi kutoa taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama
pale wanapokuwa na shaka juu ya watu ambao hawaeleweki.
“Sisi tumejipanga unajifunza kutokana na matatizo yanayompata mwenzio
kwa hiyo unachukua tahadhali kwa lile lililotokea kwa mwenzetu
nafikiri tuko vizuri ,wananchi wanatakiwa wawe watulivu kwa sasa,
lakini wanatakiwa kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama kwa mtu
yoyote wanaye mtilia wasiwasi”alisema Malemi.
Mgeni rasmi katika mkutano wa siku tatu wa wa maofisa
wanadhimu,wahasibu na maofisa mipango wa mikoa na vikosi wa jeshi la
polisi ,naibu katibu mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya chi Mwamini
Malemi akiwa ameongozana na mkurugenzi wa makosa ya jinai nchini
Robert Manumba pamoja na mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi
Moshi,Commandant Matanga Mbushi wakielekea katika ukumbi wa mkutano .
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini mada
zilizokuwa zikitolewa.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mwamini Malemi
akizungumza katika mkutano huo.
Mhasibu mkuu wa Polisi Frank Msacky akizungumza katika mkutano huo.
Hali ya ulinzi ilikuwa ni ya hali ya juu katika eneo la CCP ambako mkutano huo umefanyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...