MH. MUNDE TAMBWE MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA NA MJUMBE WA NEC AMBAYE  NDIYE MDHAMINI MASHINDANO HAYO YA KUWASAKA NYOTA WA KUIMBA, MICHEZO YA MASUMBWI YA NGUMI, KARATE, MASHINDANO YA BAISKELI, BAO NA KU-DANCE YALIYOFANYIKA  LEO KATIKA VIWANJA VYA STENDI YA ZAMANI YA MABASI. 

ZAWADI ZOTE ZIMEGHARIMU TSH 6.7 MILIONI, ZILIZOENDA KWA WASHINDI WA MBIO ZA BAISKELI, MCHEZO WA BAO, WACHEZA MUZIKI, MASUMBWI, KARATE, NA KUIMBA. MH. MUNDE AMBAYE YEYE NDIYE MDHAMINI AMEAHIDI KUBORESHA SHINDANO HILO KWA MSIMU UJAO KWA KUUTAMBUA MWITIKIO WA WATU WALIOJALI NA KUJITOKEZA KATIKA MASHINDANO HAYO.
KATIKA KUMSAKA NYOTA WA BAO.
MCHEZO WA KARATE
WASHIRIKI WA MBIO ZA BAISKELI, WAKISHINDANA KUENDESHA BAISKELI KUTOKA KIWANJA CHA STENDI YA ZAMANI YA MABASI HADI KATIKA KIWANJA CHA NDEGE NA KURUDI. WASHINDI WATANO WA KWANZA WALIKABIDHIWA BAISKELI MPYA AINA YA PHOENIX.
MWANADADA HUYU  ALIIBUKA  NYOTA WA KUIMBA NA KUKABIDHIWA KITITA CHA LAKI TATU (300,000) HUKU AKISUBIRI KUPELEKWA THT (TANZANIA HOUSE OF TALENT) KWA MAFUNZO NA KUBORESHA MZIKI WAKE IKIWA NI PAMOJA NA KUFANYA BAADHI YA KAZI ZA KIMZIKI KIMKATABA
BAADHI YA MAJAJI,PICHANI KUSHOTO NI ALLY NIPISHE, ALLY BAUCHA PAMOJA NA ADAM FUNDIKIRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. siasa zetu hapa inategemea mtu anavyoweza "kuzichanga" karata zake.....Hongera sana Mama Munde kwa kuwaleta vijana pamoja....siwezi kushangaa nyota yako kisiasa iking'ara zaidi siku za usoni!

    ReplyDelete
  2. Che GuevaraOctober 01, 2013

    Wahimize wakalime ndilo la maana zaidi! Ebo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sensei Rumadha Fundi, haya basi rudi home kwenu Chemchem pale mnarani kafundishe Karate ya kweli yenye mfumo wa kimataifa.
      Kazi kwako sensei Romi!!! Vijana wanakuhitaji huko!!!

      Delete
  3. vipaji vilivyo patikana viendelezwe, isiishie hapo hapo .

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...