Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere wa CHADEMA, katika hutoba yake fupi, aliwambia   wana DMV kuhusu swala la mchakato wa katiba pamoja na uraia wa nchi mbili na haki ya kupiga kura, aliwataka wana Diaspora wa DMV wambane Rais wa Jumuiya ya Tanzania DMV Bwna Iddy Sandaly.
Pia mchumba wa Dr Slaa Mama Josephine Mushumbuzi alitoa hotuba fupi katika Mkutano wa CHADEMA DMV Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Unirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani.
Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA, mchumba wa Dr Slaa Mama Josephine Mushumbuzi,  katika mkutano wa Tawi la Chadema DMV
Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA alipokua akitoa hotuba fupi katika Mkutano wa CHADEMA DMV katika ukumbi wa  Mirage uliopo Unirvesty Blvd. Langley Park. Maryland  Nchini Marekani.
Hii ni Hotuba fupi ya Mbunge wa Viti Maalumu, Mhe. Leticia Nyerere CHADEMA alipoongelea mchakato wa Katiba mpya na Uraia wa Nchi mbili, katika Mkutano wa CHADEMA DMV Siku ya Jumapili Sept 22, katika ukumbi wa Mirage uliopo Unirvesty Blvd. Langley Park. Maryland Nchini Marekani.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Huyu mama Josephine ni nani hasa kwa Dkt. Slaa? Hapo juu imeandikwa ''mchumba''wa Dkt Slaa na hapo hapo mnaandika "mke"wa Dkt. Slaa. Ipo tofauti kubwa Kati ya mke na mchumba. Fanyeni masahihisho

    ReplyDelete
  2. CCM Oyeeeee

    Jamani Chadema njooni CCM kwani tumeshalizungumzia suala la uraia wa nchi mbili kwenye mapendekezo ya chama , kwa hiyo kwa kifupi TUNAWAPIGANIA nyie Watanzania mlioko Nje ya NChi.


    Sasa mbona mnatuchanganya kuhusu MAHUSIANO YA DR. Slaa na huyu mama so called MSomi? Ni MKE AU MCHUMBA a.k.a BIBI TUU ? NA kwa nini HAMUOWI LAKINI kumdhalilisha mama wa watu ? au ndio anangoja NDOTO yake ya KUINGIA IKULU ifike ndio tuwe na harusi ya Rais ? hehehe mama utangoja sana pole.

    Na mama samahani sana usituonee huruma kukaa nje ya nchi hakuna alielazimishwa kama unavyofikiria wewe ni katika kutanuka kimawazo ulimwengu wa leo ni kama kijiji mama , sio watanzania tuu pekee wanaoishi nje ya nchi yao , hata mataifa mengine wapo kibaaao mpakamataifa makubwa ulimwenguni hata hao Wamarekani wanaishi nje ya nchi yao. Sasa hii usiichukulie kama kigezo cha kisiasa na kutafuta point ya kisiasa tafadhali, Tanzania hakuna mkimbizi wa shida wala wa vita ni wa Hiari na tunarudi Ujuzi nyumbani kujenga Nchi yetu. hatuhitaji huruma.

    Mmmmh Chadema kuweni serious yaani huyu ndio First Lady Msomi ??? Carolite aiseee...

    Mungu Ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Rais JK alishasema kwamba anaunga mkono uraia wa nchi mbili na waziri wake wa mambo ya ndani alishasema hivyo lakini alisema katiba itaandikwa na wananchi na ukweli usiopingika wananchi wengi hawaungi mkono kitu hicho... nyie wanasiasa msituzingue kawaelimisheni wananchi siyo kuja huku kutuona sisi punguani.. pamoja na kwamba napendelea uraia wa nchi mbili nisingependa rais ahusishwe kwenye hilo kwa upande mwingine mkimpa power hiyo anaweza kuamua nchi iwe na chama kimoja cha siasa.

    ReplyDelete
  4. mimi nina swali... mbona wanasiasa wa bongo wanaboa sana kuwasikiliza eti ndugu mgeni rasmi, meza kuu blah blah who wants to hear that????

    ReplyDelete
  5. Dk. Slaa aliiambia dunia kuwa kwa kuwa anawania kuingia Ikulu shuti aingie na mwanamke msomi ---eti, alikuwa mwanamke wa kwanza kwa mabo ya InfoTech nchini

    daharau kubwa kwa akina mama wasio wasomi; hamtakiwi kuingia Ikulu, kama First Lady!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...