Assalaam Alaykum.

Kufuatia kichwa cha habari kilichopo hapo juu, nachukua fursa hii kutoa Historia fupi ya Kijana huyu anako toka na jinsi ugonjwa alionao ulivyo gundulika mpaka hivi sasa.

Zuberi Mgeni Zuberializaliwa Mwaka 1995 katika Kijiji cha Kwale Kata ya Kwale Wilaya [mpya] ya Mkinga Mkoa wa Tanga. Alifanikiwa kumaliza Shule ya Msingi kwenye Kata yake hiyo na akabahatika kuchagulia Mwaka 2010 kuendelea na Masomo ya Sekondari ambayo ipo kwenye kata hiyo. Lakini hakuweza kuendelea na Masomo hayo kwa ajili ya Ugonjwa huo. Mwandishi wa habari hii ni Ndugu wa karibu wa Mama yake Zuberi.

Bado wanaishi pamoja na Baba mzazi wa Zuberi hadi leo na jina lake ndilo hilo Mgeni.

Shughuli wanazo fanya ni Uvuvi na Ukulima mdogo. Kipato chao ni cha hali ya chini kiasi wali shindwa kumfanyia uchunguzi Kijana wao ili wafahamu ni kipi kinacho msumbua Mtoto huyo ambaye mara kwa mara alikuwa akisumbuliwa na Tumbo hivyo kufikiria kuwa ndiyo Maradhi yanayo msibu, kwahiyo walikuwa wa kimpatia Dawa za Tumbo ambazo hazikua zikitoa nafuu ya moja kwa moja na ilibidi awachishwe kundelea na Masomo ya Sekondari ndipo hapo Mwandishi wa Habari hii ambaye wakti huo alikuwa akiishi Kisiwani Pemba kwa shughuli za Ujenzi wa Barabara alipo fahamishwa na akatoa msaada wa ushauri na fedha ili Kijana apelekwe kwenye Hospitali ya Rufaa ya Bombo Mjini Tanga kwa Uchunguzi na tiba husika Mwaka 2011 Juni.

Hapo ndipo alipo gundulika kuwa anasumbuliwa na Ugonjwa ndani ya Moyo wake hivyo Hospitali hiyo ikampa Rufaa ya Kwenda Hospitali ya Taifa ya Mhimbili ambapo amekuwa na Kliniki hadi leo.


Chakusikitisha nikuwa Madaktari wa Hospitali hiyo wameshindwa kumpa Rufaa ya kwenda Nchi za nnje kwa Matibabu kamili baada ya wao kutokuwa na vifaa au ujuzi wa Tiba hiyo, hivyo ilibidi kutafutwa njia nyengine kwenye Hospitali Binafsi ikiwemo Regency ambao baada ya utafiti wao wakasema anahitajika kwenda India kwa Matibabu na Gharama kwa kipindi hicho zilihitajika wastani wa Dola 6000 za Kimarikani sawa na Shs.9,600,000/= za Tanzania.


Zikipatikana anaweza kusafirishwa na Msaidizi wake mmoja. Maelezo Mengine kwa kina yana weza kupatikana kwa kuwasiliana na Mwandishi wa Habari hii [Mjomba] moja kwa moja kwa kutumia Nambari zifuatazo:- 0777 980492 au 0714 980492 Jina lake ni Bwana Yunus Ally Chui na Mshirika wake wa karibu ni Bwana Feisal Y. Chui Nambari yake ni 0773 449662.

Msaada wa ki Fedha unaweza kutumwa kwenye Akaunti zifuatazo: 5753735527 kwa Fedha za Kitanzania na 5753735502 kwa Fedha za Kigeni Bank ya Exim Tawi la Tanga kwa Jina la Yunus Ally Chui. Ina ambatanishwa kwenye Barua hii Picha ya Zuberi ili kuthibitisha namna gani Ugonjwa huu ulivyo mbadili Umbile lake.

 SHUKRAN
Yunus Chui.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Poleni nyote wanafamilia, tuko pamoja kwa dua. Ila mungeweka namba za M pesa, tigo pesa, airtel money na z pesa ili hata sisi tunoweza kuchangia kiwango kidogo na tuliombali na matawi ya Exim bank tukatabaruku.

    ReplyDelete
  2. sawa kabisa mtoa maoni wa kwanza

    ReplyDelete
  3. GOD blesss you wote mliotoa

    ReplyDelete
  4. Ziko asasi kadhaa zinazoweza kusaidia na mwandishi kwa vile ni msomi alistahili kuzijua kwani vijisenti vya thumni thumni vitachelewesha huduma. Lion's club na wizara ya afya pia wanaweza kukusaidia.

    ReplyDelete
  5. Watanzania wenzangu tujitahidi kumchangia ili kumsaidia mtoto huyu kama tunavyochangia michango ya harusi.jARIBU KUFIKIRIA KAMA ANGEKUWA MTOTO WAKO YUKO KATIKA HALI HII NI UCHUNGU NA MATESO MAKUBWA. MUNGU ATATUBARIKI SANA.

    ReplyDelete
  6. Natoa linanikera moyo wangu kuhusu matibanu ya India ninavyoyaona na yaliyotutokea karibuni kwa jamaa zetu watatu. Wakati mwingi si wakweli. Si dicourage kumpeleka mgonjwa India lkn wakati jitihada za kukusanya fedha zikiendelea hebu piga simu hii 0773810920 au 0655810920 umcheki huyu bwana kama yupo uende na picha ya mgonjwa mkaongee nae. Dawa zake inshallah mgonjwa huyu anaweza kupona.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...