20130904_115112_resized
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akiwa ameongozana na Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes kuelekea kwenye chumba cha mikutano katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kabla ya kukabidhi msaada wa Magodoro kwenye Hospitali hiyo.
20130904_115838_resized
Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili Bi. Agnes Jonathan Mtawa akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili katika uotaji huduma kwa wananchi mbele ya mgeni rasmi Mstahihiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa katika hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali hiyo.
20130904_120709_resized
Katibu wa Neema Womans Power Mgeni Ottow akisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa.
20130904_121628_resized
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi Magodoro 50 kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili.
20130904_122836_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi Magodoro 50 kwa Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar.
20130904_122738_resized
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akimshukuru Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes (mwenye hijabu nyekundu) mara baada ya kukabidhi Magodoro hayo.
20130904_123027_resized
Mwenyekiti wa kikundi cha Neema Womans Power Bi.Maryam Dedes katika picha ya pamoja na Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakinamama wa Kikundi cha Neema Womans Power.
Na. Mwandishi wetu.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala MH.JERRY SILAA amekabidhi magodoro 50 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupitia kikundi cha wakimama "NEEMA WOMANS POWER".
Neema Womens Power ni kikundi cha wakina mama kilichoanzishwa mwaka 2005 kwa kuanza na Madrasa mbili ya akinamama na wasichana akiwa na wanafunzi 18 tu. Madrasa hizo zipo Kinondoni na Buguruni chini ya Mwenyekiti wa kikundi hicho Bi.Maryam Dedes. Jumuiya hii pamoja na kuwa na Elimu ya dini, husaidia jamii kwa michango mbalimbali ikiwemo kulipia ada za shule kwa wanafunzi wasiokuwa na uwezo, kusaidia Walemavu na Wajane pamoja na familia duni.
Katika hafla hiyo fupi Mgeni rasmi Mh. Jerry Silaa ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuweza kujitoa kwa kusaidia jamii kwani mzigo uliopo kwa Serikali peke yake haiwezi, na ukizingatia ya kwamba hakuna mtu asiyeijua Hospitali kama si Muhimbili basi Amana, Temeke au Mwananyamala na Hospitali nyingine nyingi zinahitaji msaada vifaa mbalimbali na endapo kila mwananchi angeweza kuchangia japo kifaa kimoja sasa tungekuwa mbali sana na inawezekana kabisa tusingekuwa na matatizo sugu katika Hospitali zetu.
Mh.Jerry ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha huduma zinaboreshwa ndani ya Halmashauri yake na anayesifika kwa uchapakazi wake na umakini aliwashukuru kwa dhati kabisa uongozi wa Neema Womans Power pamoja na wanachama wao kwa kuliona tatizo hilo na kwa uwezo walionao leo hii wameweza kutoa magodoro hayo 50 na kuwaasa waendelee kujitoa zaidi na wasife moyo maana kazi ya jamii haina malipo zaidi ya fadhira mbele za Mungu.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi Magodoro imehudhuriwa na Bi.Maryam Dedes ambaye ni Mwenyekiti wa kikundi hicho, Agnes Jonathan Mtawa- Mkurugenzi wa Wauguzi Hospitali ya Muhimbili, Mgeni Ottow Katibu wa Neema Womans Power pamoja na Khadija Mwita Makamu mwenyekiti na wajumbe wao 30 na Uongozi wa Hospitali ya muhimbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. ALLAH AWALIPE DUNIANI NA KESHO AKHERA,MLIPO TOA AWJALIZIE MARA DUFU

    INSH ALLAH

    ReplyDelete
  2. Hongereni wana wa madrasa ila kumbukeni mafundisho ya dini yenu, ukitoa mkono wa kulia basi wa kushoto usione.

    ReplyDelete
  3. akina mama mko juu

    ReplyDelete
  4. Nadhani tuwape hongera hawa akina mama kwa mchango wao hasa hapo muhimbili.
    Kuhusu suala la "kutoa mkono wa kulia na wa kushoto usijue" ,kama mtoa maoni hapo juu anavyoshauri,ni inategemea na hali ilivyo .Kwa hapa ni sawa walivyofanya maana wanahamasisha jamii ili wengine wafanye hivyo,kuna wengi wenye uwezo mkubwa labda nao watapata iiman ya kutoa.
    Ni maoni yangu tu....

    ReplyDelete
  5. misaada kama hii inatakiwa itolewe kwa kuonesha hasa kama alivosema mdau wa hapo juu nadhani ni wa nne ila msaada wa kusaidia maskini huo ndio wa kujificha sio hii ya kuhamasisha....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...