Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein akikata utepe kuzindua Jengo jipya la kituo cha Jamii na watoto cha (ZAPHA+) (kushoto) Mwenyekiti wa Bodi ya wazamini wa kituo hicho Bi. Hasina Hamadi. Welezo nnje kidogo ya Mji Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein akipata maelezo kwa mshauri Nasaha wa kituo cha (ZAPHA+) Salum Ramadhan Wakili alipokuwa akiangalia baadhi ya huduma zinazo tolewa kituoni hapo.
Wasanii wa (ZAPHA+) wakionesha igizo jinsi ya watu wenye UKIMWI wanavyo fanyiwa unyanyapaa,huko Welezo katika uzinduzi wa Jengo la kituo cha Jamii na watoto cha (ZAPHA+) Mjini nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Baadhi ya wageni walikwa waliofika katika uzinduzi wa Jengo la kituo cha Jamii na watoto cha (ZAPHA+) Welezo nnje kidoga ya Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein akiwahutubia wananchi katika uzindizi wa Jengo la (ZAPHA+) huko Welezo nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhammed Shein katika picha ya pamoja na watoto wanaopatiwa huduma na (ZAPHA+) huko kituoni kwao Welezo nnje kidogo ya Mji wa Zanzibar. PICHA ZOTE NA MAKAME MSHENGA WA MAELEZO ZANZIBAR
Na Khadija khamis na
Riziki Salum Maelezo Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dkt. Ali Mohammed Shein amewapongeza viongozi wa ZAPHA + kwa jitihada zao zilizowawezesha kumiliki jengo lao endelevu la kuweza kutoa huduma bora kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Zanzibar.
Kauli hiyo alitolewa jana huko katika sherehe za uzinduzi wa jengo jipya la ZAPHA+ Kituo cha jamii na watoto kilichopo Welezo wilaya ya Mjini Magharibi.
Alisema kuwa hatua hiyo iliyofikia ni nzuri na ya kupongezwa kwa mafanikio hayo kwani ni chachu ya maendeleo kwa wanaoishi na maambukizo ya virusi vya UKIMWI katika kujiona wanajamii kuwa na chuo chao cha kupata elimu na ushauri nasaha pia ni chimbuko la matumaini kwa watoto wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI.
“Serikali inathamini juhudi zenu za jumuiya kwani inatoa mashirikiano ya pamoja kwa kupiga vita unyanyapaa dhidi ya watu wanaoishi na ukimwi,” alisema Dkt Shein.
Aidha alisema kuwa zaidi ya watoto 547 tayari waneripotiwa wanaishi na virusi vya ukimwi sawa na asilimia 68 % wakiwa wanaume 194 na wanawake 180 ambao tayari wanatumia dawa za ARV Zanzibar.
Alisisitiza kuwa iko haja ya wananchi kujitokeza kwa wingi katika kushirikiana katika kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, mayatima na wanaoishi na virusi .
Alisema kuwa iko haja kwa wananchi kukubali kubadili tabia zao na kurudi katika tamaduni zao za mila silka na itikadi za kizanzibari kuweza kupendana kushirikiana na kusaidiana kwa hali na mali .
Aliengezea kuwa wananchi katika kushikamana tupige vita juu ya utumiaji madawa ya kulevya kwani tathmini inaonyesha kuwa asilimia kubwa ya walioathirika ni vijana ambao wamejihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya .
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Consolata John alisema kuwa amemshukuru Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohammed Shein kwa kuweza kukubali mwaliko wao kwani ni ishara tosha ya kuwajali na kuwathamini sana mchango wao katika maendeleo ya jamii ya Zanzibar.
Aidha alisema kuwa juhudi kubwa zinachukuliwa katika kuendeleza jumuiya hiyo kwa kuanzisha miradi mbalimabli ya kimaendeleo ikiwemo kilimo cha mboga mboga , utengenezaji wa sabuni na mafunzo ya mapishi kwa watu wanaishi na virusi vya ukimwi.
Jumuiya ya ZAPHA + Zanzibar imeanzishwa mwaka 1994 na kusajiliwa rasmi kama asasi ya kiraiya mwaka 1996 ikiwa na wanachama waanzilishi 26 hadi sasa ina wanachama 2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...