Serikali ya Kenya kupitia kwa waziri wake wa usalama Joseph Ole Lenku imesema kuwa watu 59 wamefariki katika shambulizi la kigaidi lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab na wengine 175 kujeruhiwa. Waziri Ole Lenku amesema kuwa idadi ya magaidi walio ndani ya jengo hilo ni kati ya kumi na kumi na tano na haijulikani ikiwa wanwazulia waathiriwa au waathiriwa wamjificha katika sehemu mbali mbali z jumba la Westgate. 
 Shirika la Red Cross awali katika taarifa yake ilisema kuwa watu 43 ndio waliofariki na zaidi ya 50 kujeruhiwa huku wengine wakitekwa nyara katika mashambulizi la kigaidi Jumamosi mchana. Milio ya risasi imeweza kusikika katika jengo la Westgate mjini Nairobi Kenya, ambako wanamgambo wa Al shabaab wanawazuilia mateka ambao idadi yao haijajulikana hadi sasa. 
Wanajeshi wawili walijeruhiwa katika ufyatulianaji huo na kukimbizwa hospitalini kwa matibabu huku watu wawili wakinusuriwa asubuhi ya leo. 
 Hadi sasa jeshi limeweza kudhibiti hali nje na ndani ya jengo hilo, magari ya kijeshi yakiwa yameletwa katika eneo hilo huku polisi na wanajeshi wakijaraibu kuwanusuru baadhi ambao wangali wanazuiliwa ndani ya jengo hilo. Watu 39 wameuawa baada ya wanamgambo hao kushambulia jengo hilo mwanzo katika eneo la kuegeshea magari na kisha kuingia ndani ya mikahawa na maduka katika jengo hilo lenye ghorofa nne na kuwpaiga watu risasi kuholela. Kuna taarifa kuwa wanamgambo hao wako ndani ya duka moja kubwa katika jengo hilo. Rais Kenyatta anasema kuwa baadhi ya waliofariki ni jamaa zake. 
Miongoni mwa waliofariki pia afisa wa ubalozi wa Canada nchini Kenya, na raia wawili wa Ufaransa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...