WASHIRIKI wa shindano la Redd's Miss Tanzania leo watapata fursa ya kumjua mrembo wa kwanza kuingia katika hatua ya Nusu fainali ya Shindano la Redd's Miss Tanzania 2013 wakati mrembo mmoja kati ya wanyange hao 30 atakapotajwa mshindi wa Miss Photogenic 2013.

Shindano hilo no moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusufainali ya shindano hilo litakalo fanyika baadae mwezi ujao.

Miongoni mwa mataji hayo ni Miss Tanzania Photogenic, Miss Tanzania Top Model, Miss Tanzania Personality, Miss Tanzania Sports Lady na Miss Tanzania Talent.

Akizungumza na mwandishi wetu leo, Mkurugenzi wa Lino International Agency, Waandaaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga 'Uncle' amesema jopo la majaji watatu ambao ni wapiga picha na wanahabari wazoefu wa masuala ya urembo Tanzania watakaa na kuchagua mshindi huyo kupitia picha mbalimbali za warembo hao.

Mshindi anataraji kutangazwa leo jioni katika hoteli ya Giraffe Ocean View na kujipatia tiketi hiyo.

Taji la Redd's Miss Tanania Photogenic  linashikiliwa na Mrembo Lucy Stephano aliyelitwaa mwaka 2012. Wafuatao ndio warembo watakao wania taji hilo hii leo.

 ESHYA RASHID

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kuhakikisha ni Mrembo tunaomba wasewe na Kope bandia, Kucha Bandia,Nywele bandia,Meno Bandia,Macho bandia(yaani lens za macho za kubandika,makalio bandia,matiti bandia.

    Ili tusiwe na Mrembo Feki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...