Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goestzche akimpongeza Redd’s Miss Tanzania 2013,Hapiness Watimanywa wakati alipotembelea TBL jijini Dar es Salaam leo ili kutoa Shukrani zake kwa Kampuni hiyo ambayo ndio mdhamini Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania.Kushoto ni Mkugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas.
Mkugenzi wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Kushila Thomas akizungumza jambo na Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013,Hapiness Watimanywa.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goestzche.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Fimbo Buttala akijibu moja ya maswali ya waandishi wa habari kwenye tafrija fupi ya kumtambulisha Redd’s Miss Tanzania kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),Robin Goestzche.
Redd’s Miss Tanzania 2013,Hapiness Watimanywa katikati akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi mkuu wa TBL,Robin Goestzche na kushoto ni Mkugenzi wa masoko wa TBL,Kushila Thomas katikati yao ni kushoto kwake ni mshindi wa pili shindano la Redd’s Miss Tanzania,Latifa Mohamed na mshindi wa tatu Clara Bayo.

REDD’S Miss Tanzania, Happiness Watimanywa jana alitembelea rasmi Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) walio wadhamini wa shindano hilo, ambapo alikutana na uongozi wa juu ili kujitambulisha.

Katika ziara hiyo, Happiness alifuatana na mshindi wa pili, Latifa Mohammed, mshindi wa tatu, Clara Bayo pamoja na Kamati ya Redd’s Miss Tanzania.

Akizungumza mara baada ya kukutana na mrembo huyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBL, Robin Goestache alisema, wao kama wadhamini wakuu wanajisifu kuwa sehemu ya mafanikio ya Redd’s Miss Tanzania, huku akimsifu mrembo huyo kwa ushindi wake.

“Kila mmoja kati yetu anajua shindano lilivyokuwa gumu, warembo wote walikuwa na sifa na ninawapongeza ninyi mlioshinda na tunawakaribisha katika familia ya TBL,” alisema.

Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, Kushillah Thomas, naye alitumia fursa hiyo kuwapongeza warembo hao na kusema ana imani kubwa nao watafanya vizuri zaidi katika kipindi chao.

Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah alisema, toka waanze kudhamini shindano hilo wamepata mafanikio makubwa mno, huku kukiwa na kazi nyingi za jamii wanazozifanya na warembo waliofanikiwa kutwaa taji hilo.

Happiness naye aliishukuru TBL kwa kudhamini shindano hilo na kusema anajivunia kwa kiasi kikubwa kuwa sehemu ya familia ya Redd’s.

“Kwa kiasi kikubwa nawashukuru kutokana na kudhamini shindano hili kwa muda wa miaka 13, kwani mmesaidia mengi kwa warembo na najivunia kuvaa sura ya Redd’s.”

Shindano la Redd’s Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s Original kinachozalishwa na kusambazwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...