Muwakilishi wa NSSF-Makao Makuu Bwa,Salim Khalfan akizungumza mbele ya vijana mbalimbali waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,iliofanyika mapema leo  kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU),kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. Semina hiyo iliyoandaliwa na Clouds Media Group,imefadhiriwa na shirika la NSSF,Zantel,MaxMalipo,Lake Oil,TPSF.
 Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti,Bwa.Eprahim Mafuru akizungumza na wakazi wa Mbeya (hawapo pichani) waliojitokeza kwenye semina ya Fursa kwa vijana,filiofanyika leo asubuhi ndani ya ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU),kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.Kampuni ya Serengiti ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Fiesta 2013 linalotarajiwa kufanyika jioni ya leo kwenye uwanja Sokoine.
 Mkali wa kughani mashairi hapa nchini,Mrisho Mpoto akifafanua jambo mbele ya wakazi mbalimbali wa mji wa Mbeya,alipokuwa akiielezea mada mojawapo iliyohusiana na fursa mbalimbali zilizomo ndani ya mkoa huo namna ya kuzitumia,Semina hiyo imefanyika leo ndani ya ukumbi wa chuo cha Teofilo Kisanji (TEKU) kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya.
 Sehemu ya vijana waliojitokeza k wa wingi kwenye semina hiyo ya Fursa kwa vijana.
Mmoja wa Vijana Wajasiliamali ,ambaye ana mradi mkubwa wa kuuza juisi,Gasto Sony mkazi Uyole mkoani Mbeya,akieleza zaidi kwa vijana wenzake waliojitokeza kwa wingi kwenye semina hiyo,namna ambayo ameweza kuitumia fursa alioipata na kuwa mjasiliamali wa kuuza juisi kisasa kabisa.
  Baadhi ya vijana mbalimbali kutoka ndani ya mkoa wa Mbeya  wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi kwenye ukumbi wa  chuo cha Teofilo Kisanji kilichopo maeneo ya Block T-Mama John mkoani Mbeya. 
 Semina ya Fursa kwa vijana ikiendelea.Semina kama hii imekweíshafanyika kwenye mikoa ya Kigoma,Singida,Tabora,Mtwara na leo mkoani Mbeya.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...