Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya Royal Dutch Shell plc (Shell) kwa pamoja wametangaza uwekaji saini wa Waraka wa Makubaliano.
Waraka huo unaweka bayana ushirikiano kati ya Kampuni ya Shell na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta ya Mafuta na Gesi na inafafanua hususan kuhusu hatua za awali zinazohusiana na kujenga uwezo katika sekta ya Mafuta na Gesi pamoja na Maendeleo ya Vijana katika kukuza ujuzi wao kwenye sekta hii, ikiwa ni pamoja na jitihada za elimu na uwezo wa ujasiriamali.
Axel Knospe, Mwenyekiti wa Shell Deepwater Tanzania alieleza kuwa,Kampuni ya Shell ina nia ya kuwa na uhusiano imara na Serikali ya Zanzibar na pale itakapofaa, itaanza hatua za utafiti ambao utafanyika kwa njia endelevu, ya kiuchumi, kijamii na inayowajibika kimazingira.
Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Ramadhani Abdalla Shaaban alisema kuwa utiaji saini wa waraka huo ni hatua kubwa inayoonyesha jitihada za Serikali za kuendeleza sekta ya nishati Zanzibar
Axel Knospe, Mwenyekiti wa Shell Deepwater Tanzania akikabidhiana Waraka wa Makubaliano na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Ramadhani Abdalla Shaaban mara baada ya kuusaini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...