Hayati Wakili Israel Magesa

Ndugu, Jamaa na Marafiki !
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wote kwa jinsi mlivyoshirikiana nasi kwa hali na mali katika sherehe ya mwisho duniani ya baba yetu mpendwa Wakili Israel Magesa (RIP).

Kama familia hatuwezi kutaja majina ya watu na taasisi moja moja ila tunatoa shukrani za dhati kwa wote na kwa ujumla tunaomba mzipokee.

Marehemu alikuwa ni mtu aliyethamini watu wote na kuwasaidia zaidi wale wasio na uwezo, alithamini sana elimu na aliamini kupitia elimu basi tutaweza kuendeleza nchi yetu kwa kasi kubwa zaidi. Alikuwa ni mchapa kazi, mwenye uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa lake na siku zote alikuwa akijali maslahi ya wengi na hakuchoka kufanya kazi kwa bidii na maarifa yake yote, licha ya umri aliokuwa nao na hata siku anafariki ghafla alikuwa anaenda kazini kufanya kazi.

Hivyo basi tunaomba tuendeleze mazuri yote aliyaanzisha au aliyokuwa akiyafanya kwa faida ya jamii yetu na Taifa letu kwa ujumla.

Kila mmoja atimize wajibu wake kwa kufanya kazi kwa bidii na maarifa na kwa pamoja tunaweza kujenga Tanzania bora zaidi ya tuliyoikuta.

Mungu awabariki wote na sasa tuendelee na ujenzi wa Taifa, tudumishe umoja, mshikamano na amani kwa Taifa letu.

Mungu ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


-Phares Magesa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. RIP Advocate Magesa. Mungu aiweke roho ya Mzee mahala pema peponi, amen.

    ReplyDelete
  2. rip anko wake annah mtani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...