Askari wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania wakimdhibiti Mhe mbunge wa Chadema jimbo la Mbeya Mjini, Mhe. Joseph Mbilinyi a.k.a Sugu ndani ya bunge wakati akitolewa ndani ya ukumbi wa bunge hilo mjini Dodoma leo.
---------------------------------------------------
Vurugu kubwa zimetokea Bungeni leo  baada ya Naibu Spika kutoa amri ya kutolewa nje kwa kiongozi wa kambi ya upinzania Bungeni Freeman Mbowe ambapo wabunge wa kambi ya upinzani hawakukubaliana na amri hiyo. 
 Chanzo cha kutolewa kwa amri hiyo ni kutokana na Mbunge huyo wa Hai kusimama na kuanza kuzungumza pasipo kupewa ruhusa ili apinge uamuzi wa kura zilizopigwa na Wabunge ambapo Bunge lilipiga kura ya kuuondoa mjadala wa mswada wa katiba au ubaki ambapo wabunge 56 walisema mjadala huo uondolewe na Wabunge 159 walisema mjadala huo uendelee kwani ulishapita kwenye hatua mbalimbali. 
 Mara baada ya zoezi la upigaji kura kuisha Naibu Spika Job Ndugai aliendelea na utaratibu wa Bunge ambapo alimsimamisha Mhe. Mrema achangie mjadala na wakati huo huo Mhe. Mbowe naye alisimama kupinga uamuzi wa Naibu Spika na ndipo alipotoa amri kwa askari wa Bungeni wamtoe nje ya ukumbi wa Bunge. Mvutano mkali kati ya Wabunge wa kambi ya upinzania dhidi ya polisi ulizuka na songombingo likaumuka
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi akiwa ameng'ang'ania  Migrophone ya sehemu ya Kuzungumzia wapinzani Bungeni wakati polisi walipokuwa wakimtoa Bungeni Mjini Dodoma. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. AIBU. Amani

    ReplyDelete
  2. sasa si wamwanche aimbe sugu sugu sguuu dah Aibu ya mwaka kwa wapiga kura

    ReplyDelete
  3. Tutafika kweli na hii katiba yetu?

    ReplyDelete
  4. Michuzi Naomba video kama ipo ya tukio hili!!!! ilivyo anza mpaka mwisho nataka kujua wapi palikuwa na tatizo

    ReplyDelete
  5. This is sad and a bit embarrassing, uneducated MPs, if mwalimu sees this rubbish, he would collapse and have a heart attack.

    ReplyDelete
  6. Ni aibu kuona watu waliosoma na wanaakili kutofata sheria ya bunge,umeisha ona wapi ?bunge la Tanzania limekuwa ni la wauni tuu na kama ni hivyo Chadema mtaweza kutawala nchi huu ni uhuni na aibu kwa Tanzania tunakoelekea si pema kama hatutaweza kujuwa maana ya bunge ni aibu mr sugu nilikuwa nafikiria ulipokuwa hapa uk miaka ya nyuma ulijfunza kumbe ni bure ,

    mr masanja

    ReplyDelete
  7. Indonesia ngumi zinaruka inapobidi kutetea maslahi ya Nchi. Tupo pazuri!

    ReplyDelete
  8. Hapa tunaenda pazuri tu. wenye akili tunaona wapi kuna tatizo. Bunge linasahau kuwa ni kwa ajili ya taifa zima si kwa ajili ya ccm tu . Hapa ndo kuna tatizo. Mimi si mwanachama wa chama chochote, lakini naweza kusema wabunge wa pande zote wana walakini. Mbubge huwezi kusimama nadani ya bunge na kuanza kutusi wabunge wenzio. Pili, kama mwenyekiti anasema fanya hivi ni lazima ufanya hivyo pia.

    Hapa mimi sioni mwenye nafuu. Alhamisi tulishuhudia Mh Mbowe akikataa kuketi, haya....tulishuhudia Mh.. Ndugai akiwaambia maaskari wakae tayari kwa kitakachotokea....haya.... Sugu alivyopigwa na kubebwa juu juu kutupwa nje kama mzoga...alipojitetea kwa kulipiza ikawa issue akaanza kutafutwa na polisi.

    Hapa najiuliza. Bunge zima limekosa mtu mwenye busara?

    ReplyDelete
  9. Hapa ndio tuta thibitisha Vigezo vya kuchagua WAHESHIMWA WABUNGE:

    Sanaa ya Muziki na Ubunge wapi na wapi?

    ReplyDelete
  10. Huu Ukumbi wa Masumbwi ama Ukumbi wa Bunge?

    KAZI TUNAYO NA MATAAHIRA BUNGENI, PANA UMUHIMU WA KUWAPIMA AFYA ZA AKILI WAHESHIMIWA WABUNGE MUDA HADI MUDA !!!

    INAWEZEKANA MTU AKAINGIA BUNGENI AKIWA MZIMA WA AFYA NA BAADA YA MUDA KAMA BINAADAMU AKAWA MTAMBO, NDIO HAYA TUNAYAONA SASA.

    Badala ya kuwashusha watu kwenye Majukwaa ya Muziki na kuwa ingiza kwenye Kumbi za Mabunge si afadhali tunge ingiza kupitia Viti Maalum Wazee wa Baraza wenye busara na hekima zao wa Mahakama za Mwanzo?

    ReplyDelete
  11. NAIBU HAKUWA NA SABABU YA KUWAITA ASKARI NA KUWAPA AMRI YA KUWATOA WABUNGE KWA NGUVU NA KUWABURUZA NJE NAMNA HIYA!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  12. Duuuh hali tete.... tunapoelekea sasa ni wabunge kupigana risasi bungeni.ila ndo shida ya kuwapa vijana furswa ya kuendesha nchi wakati bado wanahamu ya kuvuta bangi.

    ReplyDelete
  13. Hivi CHADEMA mnatupeleka wapi, watoto, wake zenu na wapiga kura wenu wanawaona mkifanya upuuzi huu Bungeni, mkipewa serikali itakuwaje!!! Watanzania tafakari na mchukue hatua. Wanangu wanawaita John Cena

    ReplyDelete
  14. Aibu? Hasha li Lah
    If it were only aibu, I could live with it, but this is something else.This man a degree below ..... who managed to fool people to vote for him and his party to serve them. Atimuliwe na akatafute kazi ya ubaunsa.

    ReplyDelete
  15. Tatizo ni letu wapiga kura,Tanzania kitu chochote cha kudanganya jamii,tayari huyo anafaa kuwa Rais,nadhani maendeleo yetu ayawezi kuja kwa mtindo huu,chama kinachoongoza kazi yake ni kusamia yaliyo ,ktk mabunge yote duniani ,kura ndiyo msema kweli mbungeni ,mbowe hataki,huyo sugu anatumia nguvu nyingi sana huko bungeni ni vema hizo nguvu azielekeza kwenye muziki ,ndiyo molla kitu alichomubaliki nacho,ajiulize je anaona anafaa kuwa kiongozi au mwanamuziki,jibu mwamuziki,siasa bado du,gumi tena?

    ReplyDelete
  16. A big shame kwa mbunge wangu sugu anayeniwakilisha. Chadema nakupenda, ila sasa imekuwa too much kwenu, mnaonyesha hamuwezi shika nchi. mnafanya vitu kama mna hang over vile,,,maskini kura yangu ya 2010 kwa sugu....daah...najutaaaa...

    ReplyDelete
  17. Mtazamo wangu nikwamba naibu spika analichukulia kiwepesi suala la katiba bila kukumbuka kuwa katiba ndo injini ya nchi yoyote tuwe makini sana hapa

    ReplyDelete
  18. MADECHA CHADEMA HAMFAI WOOOOTE tuachieni nchi yetu ya amani

    ReplyDelete
  19. kama kura zilipigwa bungeni na wengi wakashinda sasa mbowe mbona anapinga democracy ambayo wote tulidhani ndio anaitetea? aah sasa unanifanya nianzekujiuliza upyaa kama nipo sahihi kukufuata kiongozi wangu dah!

    ReplyDelete
  20. mi sishangai kuona hivyo, mbona hapo karibu Kenya tu watu wanachapana makofi sembuse hapa...

    watiane na mangumi haiwezekan bunge liwe la watu wamoja tu, kuna maana gani kuwa na vyama tofauti kama ni hivyo!

    ReplyDelete
  21. mi sishangai kuona hivyo, mbona hapo karibu Kenya tu watu wanachapana makofi sembuse hapa...

    watiane na mangumi haiwezekan bunge liwe la watu wamoja tu, kuna maana gani kuwa na vyama tofauti kama ni hivyo!

    ReplyDelete
  22. Kabla ya kuhukumu Tujue shida ilikuwa wapi! Kisha tuhukumu ama zaidi ya hukumu TUTOE MWANGA KO SIKUZIJAZO TUNATOKAJE HAPO!!
    Tu wepessii kuona vibanzi kwa wenzetu!! wAKATI WENYEWE TUNA 'MIBORITI'

    ReplyDelete
  23. niaibu kubwa sana

    ReplyDelete
  24. niaibu kubwa sana

    ReplyDelete
  25. Dah Mungu kawe kiongozi wetu maana viongozi wetu wameshindwa kutuongoza, Mungu ibariki TANZANIA

    ReplyDelete
  26. Unajua hapo wewe nikwamba watu wengi wameona tu sugu anatolewa nje kwa nguvu lkn ukweli wenyewe watu hamtaki kuujua hapo ndio shida inapokuwa ,kuna uwezekano mkubwa sugu akawa anapigania kitu sahihi kabisa!! mabunge mengi tu watu wanapigana kabisa unajua,jaribuni kufuatilia hata kimataifa na sio kuangalia bunge la nyumbani,sugu anaweza kuwa yuko sahihi,kwani anaona kabisa ndungai anazingua wakati anachosema ni cha ukweli,,wabunge wa ccm wenyewe wengi hawajui umhimu wa katiba wapo mle ndani tu kama mabenchi tu,sasa hapo,mfikirie sugu atakuwa anapingwa lkn yuko sahihi,kila siku kulia nchi inakufa masikini kumbe walio wengi matatizo baada ya kutaka kujua chanzo hamtaki mnarukia mambo mwishoni wengi mnajua kama sugu alikuwa sahihi au sio?,,lini mkombozi wa nchi akaacha kupingwa ..hata yesu aliteswa na aliowasaidia,baada ya kumuunga mkono mnakuja na point sa kivyama,,hamwezi kufanya maisha bila kutegemea hela za kupewa kipindi cha kampeni nini,kuweni makini wakubwa.

    ReplyDelete
  27. Hali ilivyokuwa
    Hali ya machafuko ndani ya Bunge ilitokana na baadhi ya wabunge wa vyama vyote kuomba mwongozo wa Spika kwa ajili ya kumtaka aondoe majadiliano ya muswada huo.
    Wabunge hao walidai muswada huo ulikuwa haujakidhi mahitaji ya utoaji maoni hususan kwa upande wa Zanzibar.
    Miongozo hiyo ilimfanya Naibu Spika, Job Ndugai, kukubali hoja ya kupigwa kura ya kuwahoji wabunge wanaotaka muswada huo uondolewe.
    Hata hivyo, mbunge wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) alimtaka Spika kuruhusu upigwaji wa kura za mtu mmoja mmoja badala ya kutumia kura jumla ya ndiyo au siyo.
    Ndugai alikubaliana na Mnyika na kuruhusu kupigwa kura kwa kuwaita majina wabunge na wale waliosema ndiyo walimaanisha muswada uondolewe na wale waliosema siyo walimaanisha uendelee.
    Alibainisha kuwa wabunge waliotakiwa kupiga kura ni 351 ambapo 136 hawakuwepo na waliopiga kura ya siyo walikuwa 156 na ndiyo 59.
    Ndugai alisema waliokuwa wakitaka hoja hiyo iondolewe wameshindwa hivyo alianza kumpa nafasi mbunge wa Vunjo, Augustine Mrema (TLP) kuchangia.
    Hata hivyo kabla ya Mrema kuzungumza Mbowe alisimama kuomba mwongozo wa kiti lakini Ndugai alikataa na kumtaka aketi chini na hivyo kumruhusu Mrema aendelee.
    Hatua ya Mbowe kunyimwa nafasi wakati kanuni za Bunge zinaruhusu kiongozi huyo kupewa nafasi wakati wowote anaposimama, iliwafanya wapinzani kusimama wote kumpinga Ndugai.
    Ndugai katika kujihami kibabe alipoona hali hiyo, aliwaomba askari wa Bunge kujiandaa kwa dakika tano na kama mambo hayatatulia atawaruhusu waingie ndani ya ukumbi wa Bunge.
    Baada ya hali kutotulia, Ndugai aliwaita askari waingie ukumbini ili wamtoe nje Mbowe jambo lililozidisha tafrani kwa wabunge wenzake kumkinga asiguswe.
    Mbunge wa Mbeya, Joseph Mbilinyi, Silvester Kasulumbayi (Maswa Mashariki), Moses Machali (Kasulu Mjini) waliwaongoza wenzao kuwazuia askari wasitekeleze agizo la Ndugai.
    Askari hao walilazimika kusubiri kwa muda usiopungua dakika tano huku wakifanya majadiliano na wapinzani juu ya kumtoa nje Mbowe.
    Wakati hali hiyo ikiendelea, Ndugai alikuwa amesimama kwenye kiti chake huku akizuia vipaza sauti vya wabunge visifanye kazi ili matusi na kejeli visisikike.
    “Askari hamjaja hapa ndani kwa majadiliano nataka mara moja mwondoeni kiongozi wa kambi ya upinzani na ni lazima aondoke ndani ya ukumbi huu,” alisisitiza.
    Askari hao walilazimika kumwondoa mzobemzobe Mbilinyi huku wakimkwida na kumwangusha chini.
    Wakati Mbilinyi akitolewa nje, Kasulumbayi aliwadhibiti askari waliokuwa wakitaka kumuondoa Mbowe barabara wakashindwa kumtoa.
    Wabunge wengine John Mnyika (Ubungo), Machali (Kasulu Mjini) na Moza Abeid wa CUF Viti Maalum, walizongwa na askari hao ambao mmoja wao alimvua hijabu mbunge huyo.
    Baada ya vurugu kuwa kubwa zaidi ya dakika 30, Mbowe aliamua kutoka mwenyewe ndani ya ukumbi akifuatwa na wabunge wengine wote wa vyama vya upinzani vya CHADEMA, CUF na NCCR-Mageuzi huku Mrema wa TLP akibaki na CCM.
    Nje ya Bunge
    Hali ilizidi kuwa tete nje ya Bunge, ambapo wapinzani walikuwa wakiwatuhumu askari kwa kukubali kuwa sehemu ya CCM.
    “Usalama ni CCM…usalama ni CCM, usalama hautoinusuru CCM, 2015 tuwanawang’oa CCM…usalama mtaenda wapi?” walihoji.
    Wakiwa nje ya viwanja vya Bunge, askari waliongezwa wakiwa kwenye magari mbalimbali ambapo walimuomba Mbowe aingie kwenye gari ili hali itulie.
    Hata hivyo, Mbilinyi aliamua kumvaa mmoja wa askari aliyemtuhumu kumpiga wakati akimtoa ndani ya Bunge.
    Vurugu hizo zilipungua baada ya Mbowe kuamua kuingia kwenye gari lake na kuwataka wabunge wenzake wamuingize Mbilinyi kwenye gari hilo pia

    ReplyDelete
  28. Where we go Tanzania? (wananchi wake up……………..PLEASE, it’s for us & our country)
    Mmh? It’s ashamed, WHERE WE GO TANZANIA, if still continue to select those kind of leaders, for what was happen bungeni jana kuhusiana na issue ya katiba mpya, inapunguza thamani ya viongozi tulionao, uelevu, uvivu wa kutotaka kufikiria, kutojifunza kusikiliza, kuelewa na kuajdili kwa njia nzuri na salama kwa kutumia elimu walizonazo, busara, na heshima, sio tu kwa bunge pekee bali hata kwa wananchi waliowachagua, kwa kua bila wananchi wasingeweza fika walipo sasa,
    Ni kitendo cha aibu kwa upande wa vyama pinzania, Ni kama kuwavua nguo wananchi wake waliowachagua na Taifa kwa ujumla kwa kua si Tanzania pekee wanaofuatilia Bunge tukufu la Tanzania. WANANCHI INABIDI KUAMKA NA KUJARIBU KUCHAGUA VIONGOZI BORA NA SI BORA UONGOZI, au kufuata ushabiki na makelele ya kipindi cha uchaguzi, na we are about of having new election, TAFADHALI EBU TULIANGALIE HILI KWA UNDANI.
    I think Wabunge wanajisahau na kueka personal life katika maisha ya wananchi wale waliowachagua na wasio wachagua,ila kwa kua tayari wako katika nafasi hizo, ni viongozi wetu, tumewakubali na tuliamini wataleta changamoto za kimaendeleo kwa kutumia nyadhifa walizonazo, elimu, ufahamu wa kuchanganua na kujadili kiufasaha bila kupigana wala kutumia lugha za matusi, kwa uelevu nilionao kila sehem kuna taratibu zake endapo kama mtu atafanya kitu tofauti kutokana na sheria, taratibu zilizowekwa lazima zifuatwe, hiyo ni heshima ambayo Bunge la Tanzania linastahili kua nayo. kutokana na suala hilo basi huyo mtu ataonekana ameelimika na anaitumia kiusahihi elimu yake, busara alizo nazo na heshima kwa wananchi wake.
    Siamini ule msemo usemao kila alienda shule basi ameelimika, la hasha… inategemea na vile ambavyo utavyoitumia elimu yako ili uweze kuisaidia jamii bila kuleta matokeo mabaya ambayo yataathiri jamii kwa ujumla. Naamini sifa za kiongozi bora ni yule ambae anaweza kutatua tatizo au matatizo kwa njia ya mazungumzo bila kuleta athari katika jamii na nchi, kutumia vema elimu aliyo nayo, kujali maslahi ya Nchi na wananchi wake bila kuingiza maisha binafsi, kujadili na kuchambua kiufasaha tatizo na kutafuta njia sahii, kulitatua tatizo hilo, heshima na busara inahitajika katika kujadili mambo na kutatua matatizo kwa kua kila mmoja anauwezo wake wa kufikiria, kuchambua mambo kwa aina yake, nafikiri wabunge ebu saidianane kwa hilo, kwa kua kila siku ni siku ya kujifunza katika maisha ya mwanadamu.Wabunge shirikianeni na mueke siasa pembeni ili kujenga Tanzania bora na endelevu.
    Wananchi wa Tanzania tafadhali, anglieni hili kwa jicho la tatu, ni kweli tunahiji mabadiliko, na siku zote mahala popote pate pale mabadiliko hayatokei kwa mara moja, huchukua mda kiasi, ila inatakiwa viongozi wetu wajitoe, wawajibike, waheshimu majukum yao kwa ajili ya maendeleo endelevu ya nchi na wananchi, wafanye kazi kwa kujitoa na watekeleze yale wanayojadili na sio kuishia katika majadiliano na nyaraka, tufanye kazi kutokana na mipango tuliopanga kufuata mda sahihi uliopangwa.Sio tu kwa wanasiasa hata kwa viongozi waliopo katika mashirika ya umma, wakala wa serikali na wizara kadhalika.Tuwe na taratibu za kufuatilia kinachohitajika kufanyika, kuchambua kujua kazi ilipofikia, changamoto, ili kuweza Kujenga Tanzania bora na endelevu.Naamini inawezekana, Pamoja tunaweza.

    ReplyDelete
  29. Halafu Chadema mnataka Serikali!

    Mmepanga Sugu awe na kazi gani mkishika?

    Hivi ndivyo mtakavyo endesha nchi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...