Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) ina utaratibu wa kushirikiana na jamii zinazozunguka hifadhi, ikiwa ni pamoja na asasi za kiraia, taasisi za serikali, mahospitali, mashule, na vijiji kote nchini kwa kuchangia katika shughuli zao za maendeleo.  Michango inayotolewa na Mamlaka inalenga kuwawezesha wananchi kupitia vijiji, asasi, ama taasisi husika kwa kusaidia miradi mahususi iliyoainishwa kupitia maombi yao kwa Mamlaka na kupitishwa ofisi ya Mhifadhi Mkuu.

Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inatoa misaada hiyo kama sehemu ya majukumu yake ya kushirikiana na wanajamii (corporate social responsibility). Aidha, Mamlaka imeendelea kutoa misaada hii kwa kutegemea uwezo wa kifedha, mkazo mkubwa ukiwa kwenye miradi ya Jamii zinazozunguka hifadhi, na vilevile, kusaidia miradi, majanga, na shughuli zingine kote nchini.  Kulingana na maombi na uwezo wa fedha wa Mamlaka.

Hivi karibuni kumetokea taarifa potofu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kjamii kwamba Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inatoa msaada hiyo kwa baadhi ya Taasisi kwa mashinikizo ya kisiasa, taarifa ambazo hazina ukweli wowote na zina lengo la kufarakanisha Mamlaka na Wananchi ambao wamekuwa wakipokea misaada ya kibinadamu na kimaendeleo kwa kupitia utaratibu wa ujirani mwema wa Mamlaka. 

Habari hizi zinasikitisha, na si sahihi.

 Tunapenda kutoa rai kwa umma kwamba Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro itaendelea na jukumu lake la kusaidia jamii mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo, na kuwanusuru wananchi pale ambapo majanga yanatokea kama ilivyokuwa katika milipuko ya mabomu iliyotokea katika Jiji la Arusha hivi karibuni.
  
KAULI MBIU YETU
“UTALII UANZE NA MTANZANIA KWANZA”
Imetolewa na Kaimu Mhifadhi

MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni lini Watanzania tutajifunza kukubali makosa? NCAA kutoa pesa kupitia kwenye tasisi (NGO)ya kiongozi wa nchi (mbunge) badala ya kupeleka pesa hizo moja kwa moja kwa wananchi ni jambo lenye mazingira tatanishi. Kwani mbunge hawezi kutumia wadhifa wake kuishinikiza serikali kuwaletea wananchi maendeleo bila kupitishia fedha kwenye NGO yake? Hana sababu basi ya kuwa kiongozi. Kusema kwli viongozi wa Tanzania mnatuchosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...