Mmoja kati ya washindi 13 wa zawadi kutoka kampuni Banana Inestment ltd Adelard Kiwelu aliyejishindia zawadi ya saa. Kushoto kwake ni mkurugenzi wa kampuni hiyo Adolf Ollomi.
Mshindi wa pili wa zawadi kutoka kampuni ya Banana Investment Ltd ya jijini Arusha Elisamia Loti mkazi wa Kahe wilaya ya Moshi Vijijini akikabidhiwa seti ya Televisheni toka kwa meneja masoko wa Kiwanda hicho David Damian.
Washindi wa zawadi wakati wa mkutano wa kampuni ya Banana Investment na mawakala wa bidhaa zake wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya mawakala wa kampuni ya Banana Investment wakifuatilia houba ya mkurugenzi wa kampuni hiyo Adolf Ollomi (hayupo pichani)akati wa mkutano wa mawakala hao na viongozi wa kampuni hiyo uliofanyika katika ukumbi wa CCM mkoani Kilimanjaro. Habari na picha na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii.Moshi.
KAMPUNI ya Banana Investment ya jijini Arusha imesema itaitumia kampuni ya Majembea Auction Mart and Court Broker kufanya operesheni ya kuwakamata watengenezaji wa pombe za kienyeji ambao wamekuwa wakitumia vifungashio vya kampuni hiyo zikiwemo nembo pamoja na makasha kuweka bidhaa hafifu.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Adolf Ollomi aliyasema hayo jana wakati wa mkutano wa mawakala wa kampuni hiyo pamoja na viongozi,mkutano ulioenda sanjari na utolewaji wa zawadi kwa washindi wa mauzo wa bidhaa za kampuni hiyo kwa mkoa wa Kilimanjaro.
“Tunampango wa kuwatumia Majembe kwa ajili ya kuwakamata wote wanaotengeneza pombe za kienyeji na kisha kuziweka katika chupa na makasha yetu kwa lengo la kuwaaminisha watumiaji wa kinywaji hicho kuwa ndicho halisi kutoka katika kiwanda cha Banana.”alisema Ollomi.
Aidha Ollomi alisema asilimia 90 ya watengezaji wa pombe za kienyeji hawajathibitisha bidhaa zao TFDA hali inayochangia kuongezeka kwa watengenezaji wasiojali viwango kwa lengo la kulinda afya ya mtumiaji na kwamba wamekuwa wakiuza bidhaa zao kwa bei ya chini.
“Bidhaa yoyote kwa ajili ya kula ama ya kunywa ama imetengenezwa ndani ya nchi ama nje ya nchi lazima ithibitishwe na TFDA kabla ya kuruhusiwa kuuzwa katika soko la Tanzania,kwa watengenezaji wa pombe
za kienyeji asilimia 90 hawajaenda kuthibitisha bidhaa zao.”alisema Ollomi.
Alisema iwapo vyombo vya serikali vinahitaji kutunza afya ya wananchi wake ni wajibu wake vyombo husika kuwatafuta watengenezaji wa pombe za kienyeji wathibitishe kama zinastahili au kama hazistahili wazuiwe
kuendelea kutengeneza.
“Tunafahamu wengi wao si rasmi kwa sababu hawajajisajili katika vyombo husika kama vile vya kulipa kodi na leseni hivyo gharama zao za uendeshaji zinakuwa kidogo kutokana na kwamba hawalipi gharama zile stahiki kwa vyombo husika.”alisema Ollomi.
Alisema kutokana na kutokuwa na gharama katika uzalishaji wao hali hiyo hupelekea kuuza bidhaa zao kwa bei ya chini hatua inayochangia kutokuwepo kwa ushindani sawa katika soko la bidhaa hizo kwa watengenezaji wengine wanaofuata sheria.
Naye meneja masoko wa kampuni hiyo David Damian alisema Banana investment imetoa zawadi kwa mawakala waliofanya vizuri katika mauzo mkoa wa Kilimanjaro ambao mshindi wa kwanza alizawadiwa seti ya Tv(Flat screen) wa pili akizawadiwa Seti ya Televisheni ya kawaida huku wa tatu akiambuli baiskeli na washindi wengine walipatiwa Saaa za ukutani.
Kampuni ya Banana Investment ltd ina shughuli gani ambayo ndiyo shughuli-mama (yaani core-activity)?
ReplyDeleteMaana taarifa haisemi kama wanatengeneza Pombe ya kienyeji ya Mbege au Togwa au soda n.k!!
Mdau
Globu ya jamii
Hongera sana Kaka Olomi! You are a true entrepreneur. Keep growing and please write your case for youth to emulate the: innovation; risk taking; perseverance; hard work; professionalism and and and that you have put into your business for it to be what it is now.
ReplyDeleteCongratulations.