Katibu wa Taswa Jijini Arusha,Mussa Juma akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana Tamasha la Taswa linalotarajiwa
kufanyika kesho katika kiwanja cha general tyre,jijini humo.Kushoto ni Afisa wa Kinywaji cha Vita Malt ambao ni sehemu ya wadhamini wa Tamasha hilo,Deogratius Katambi.
Na Woinde Shizza,Arusha
Tamasha la michezo la waandishi wa habari za Michezo nchini (TASWA) linatarajiwa kufanyika
kesho September 8 katika viwanja vya general tyre vilivyopo njiro
jijini hapa.
Akiongelea tamasha hilo katibu wa chama cha waandishi wa habari za
michezo mkoani wa Arusha,Musa Juma alisema kuwa maandalizi ya tamasha
hilo yamekamilika na jumla ya timu 12 zinatarajiwa kushiriki katika
tamasha hilo.
Alisema kuwa michezo mbali mbali itachezwa katika tamasha hili ikiwa
ni pamoja na kufukuza kuku,kukimbia na magunia,mpira wa miguu ,mpira
wa pete pamoja na michezo mingine mbalimbali sambamba na burudani
mbalimbali za muzikikutoka katika sehemu na bendi mbalimbali.
Alisema kuwa hili nitamasha la nane kufanyika na kwa mara hii
wameboresha zaidi kwani zawadi zimeongezeka tofauti na kipindi
kingine.
Amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza katika tamasha hili kwani
tamasha hili ni lakihistoria kutoka na waandishi mbalimbali kushiriki
kutoka katika mikoa mbalimbali.
Alitaja baadhi ya timu zitakazo shiriki katika tamasha hili kuwa ni
pamoja na timu ya taswa ya jijini dar es salaamu ambapo inatarajiwa
kuwasili leo timu ya taswa arusha ambao ni wenyeji wa bonanza
hili,timu ya taswa manyara ,timu ya triple a fm ,sunrise fm,radio five
pamoja na timu nyingine nyingi ikiwemo timu ya tbl ambao ni wathamini
wakuu pamoja na timu ya wazee klabu.


.jpg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...