Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene akitoa ufanunuzi kwa waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam juu ya taarifa zilizochapishwa na gazeti la Malawi News kuwa Wamalawi waishio nchini Tanzania wanaogopa kutoka nje kutokana na ubaguzi wanaofanyiwa na Watanzania taarifa ambazo sio kweli.
Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Bw. Assah Mwambene akiwaonyesha waandishi wa habari jana mjini Dar es salaam kichwa cha habari cha gazeti la “Malawi News” kinachosemeka “MALAWIANS FACE XENOPHOBIA IN TZ” ambacho kilichapishwa na gazeti hilo kuhusu madai ya kubaguliwa raia hao wa kutoka Malawi jambo ambalo sio kweli.
Na Benedict Liwenga-MAELEZO_Dar es salaam
SERIKALI ya Tanzania imekanusha taarifa zilizochapishwa na gazeti la nchini Malawi lijulikanalo kama “Malawi News” kuwa Wamalawi waishio nchini Tanzania wamekuwa wakiogopa kutoka nje kutokana na ubaguzi wanaofanyiwa na Watanzania.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Serikali ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene amesema kuwa taarifa hizo ni za kupotosha umma na kuleta chuki dhidi ya Tanzania na nchi jirani na hazina ukweli wowote ule.
Bw. Mwambene ameongeza kuwa hakuna raia yeyote wa kutoka Malawi aliyebakwa wala kunyanyaswa kwa namna moja ama nyingine.
“Hakuna mwananchi yoyote kutoka Malawi aliyebakwa , wala hakuna raia yoyote wa Malawi aliyepo hapa nchini anayeogopa kutoka nje kwa sababu ya ubaguzi wowote ” amesisitiza Mkurugenzi huyo.
Amesema kuwa licha Tanzania kuwakamata wahamiaji haramu 1030 kutoka Malawi, Serikali ya Tanzania iliwapa fomu ili kama walikuwa wanahitaji kuishi nchini wahalalishe uwepo wao hapa Tanzania kwa wale wote walionyesha nia ya kuendelea kuwepo hapa nchini .
Aidha wahamiaji wote haramu 1030 kutoka Malawi waliachiwa huru na wanaendelea kukamilisha taratibu za kuhalalisha uwepo nchini.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa mpaka sasa kati wahamiaji haramu 1030 hakuna aliyewekwa ndani ama kushikiliwa na vyombo vya dola kwa kosa la kuwepo kinyume.
Kufuatia taarifa hizo ,Mkurugenzi huyo amelitaka gazeti hilo kusahihisha taarifa hiyo na kuiomba radhi Tanzania kwa upotoshaji huo na kuongeza kuwa kauli hiyo ni sawa na matusi kwa Tanzania.
Aidha amesema kuwa hadi hivi sasa zaidi ya wahamiaji haramu 24,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokarisia ya Kongo (DRC) , Rwanda, Burundi , Uganda na Zambia wamerejeshwa makwao kwa kosa la kuishi Tanzania bila vibali.
Hivi mpaka mh Raisi kuingilia kati kwa swala la wahamiaji hara Idara husiaka inatumia fedha za umma katiaka kazi zake za kila siku ikifanya nini? kuna nini katika idara zetu jamani????
ReplyDeleteUtaliombaje gazeti la nje liombe radhi? Ya hapa mjini tu hayaombi radhi!! Tujibu hoja ya upotoshi tu. usingoje radhi. Wanapotosha kwa makusudi kuuza!!
ReplyDeleteMm nashindwa kuelewa kabisa hivi sisi watanzania nani katuloga jamani? Hivi ni nn maana ya muhamiaji HARAMU nijuavyo mm mtu akiingia katika Nchi ambayo siyake bila ya kufuata sheria ya ile Nchi hili ni kosa kubwa sn,sasa hivi tunavyo ambiwa eti wamekamatwa kisha wameachiwa na wameulizwa eti kama wanataka kuishi hapa wajaze form za kuishi hapa Tanzania sasa swali la kujiuliza hapa hivi ni nani alietakiwa kufuata shelia za Nchi yetu hata kabla hawajaingia katika Nchi yetu, jamani ndugu zangu watanzania jibu liko wazi kwamba niwao hao hao WAHAMIAJI HARAMU,wafuate shelia za Nchi yetu kabla ya kuingia,sasa why watu waliovunja shelia za Nchi yetu kisha wanapewa FORM za kujaza eti kama wanataka kuishi hapa wazijaze hizo Form,hapa kishelia ilitakiwa Waludishwe kwao moja kwa moja coz washakua na makosa ya kuingia Nchini bila ya kufuata shelia za Nchi yetu na hakuna vinginevyo, RAIS WETU AMELIONA hili tatizo ambalo limesababishwa na watu wa Uhamiaji kwa uzembe wao wenyewe,na kulitolea maagizo ya kuwaondoa WAHAMIAJI HARAMU wote lakini bado watekelezaji wa hili agizo,yaonekana kama hawazijui SHELIA ZA UHAMIAJI,mm naomba watu wa uhamiaji mwende SOUTH AFRICA mkajifunze kwajinsi wanavyo kamata wahamiaji haramu na kuwaludisha makwao,sisi kinachotuponza hapa kuwaajiri watu wasiozijua shelia za UHAMIAJI,mchotakiwa kufanya kuanzia sasa mkiwakamata wahamiaji haramu ambao siku walipoingia hawakufuata shelia waludishwe makwao la sivyo iposiku tutakuja kujuta,naitwa mdudu KAKAKUONA alie wahi kuishi south africa lakini kwa sasa nipo huku UINGEREZA,nawapenda woote ndugu zangu wakitanzania huko nyumbani amani kwenu na Taifa letu,
ReplyDeleteMmeanza kupaparika sasa baada ya kuona mnarushiwa makombora everywhere hasa toka Malawi na Rwanda. Mnahitaji kupiga debe pia ili kutetea mnachokifanya. Otherwise ni kweli sifa ya TZ inaanza kunuka sasa hivi. Mimi hata sioni kwa nini manafukuza wahamiaji wanyonge kama tunaovyowaona katika picha na video humu katika internet. Ni wazee tupu, wanawake, na watoto. Na wala sio dangerous hawa. Hao majangili mlosema ndo wanaleta shida huko kagera wako wapi?? Vyombo vya wenzenu nchi jirani vinatumia internet vizuri sana kuenza propaganda- na kweli ukiangalia hizo taarifa, picha, na video za wanaofukuzwa yaana kweli unafadhaika rohoni. Nadhani hata kama rais angeona naye angesema -hey jamani hawa si wale majambazi nilioagiza wasakwe na kufukuzwa!!!. So Tz ni lazima i-run an article kwenye paper na internet everyday kuielezea story hii in a positive way. Tunataka kuona video, picha, etc zikionesha positivity on this. Otherwise STOP kufukuza wanyonge hawa.
ReplyDeleteJuzi tilikanusha ya Burundi, leo Malawi. Kuna Kesi ya Rwanda. Uganda na Kenya. Suala la EAC nalo linavukuta. Jamani mbona sura na haiba ya ujirani mwema inaanza kuondoka? Mh. Membe vipi?
ReplyDeletelisemwalo lipo watanzania bado tupo nyuma sana hii dunia ya ushirikiano sio kujitenga sasa kila nchi jirani inatutenga kwa roho zetu mbaya, na kujidanganya, tubadilike jamani haya maendeleo machache tuliyopata ni kutokana na watu kuishi nje na kuona watu wanavyoshirikiana, wale wenzangu na mimi tutabaki na kupiga kelele without solution ya maendeleo.na hatupendi kuambiwa ukweli
ReplyDeleteila ni kweli Wamalawi waishio mitaa ya Mwananyamala na Kinondoni wanafanyiwa uhuni na kporwa na majambazi. Nyumba zliingiliwa na Wamalawi tu ndio waliporwa.
ReplyDeleteSafari hii Msemaji wa serikali umekuja vizuri kwa data na taarifa.
ReplyDeleteIla pia inabidi taarifa hizi uzitoe kwa Ki-Inglishi pia ili watu wa nje kama Malawi, Umoja wa Mataifa waelewe kipi kinachojiri kuhusu wakimbizi/wahamiaji haramu wa wa Burundi, Rwanda, Malawi n.k
Pia zingati habari kuwa jijini DSM, kitongoji cha Mwananyamala raia wa Malawi wanasumbuliwa kama mdau aliyetoa commenti hapo juu..
Wamalawi hao inawezekana wengine wapo hapa kusomesha Kiinglishi ktk shule zetu, nendeni mkawahoji Wamalawi hao na tundika video ktk intaneti/mitandao.
Mdau
Taarifa+data
Hizi ni dalili za tatizo kubwa linalofukuta!! Kuna kirusi cha siku nyingi hapa kinafukuta. Sio kuwa tu tunaanza chokochoko na Wageni wa nje, ndani ya nchi wakulima na wafanyakazi wanafarakanishwa,Tembo na Simba hawana usalama, na wanyama wengineo. Walemavu wa ngozi nao kasheshe haijatulia, bado matumizi ya acid kwenye miili ya binadamu, rasilimali asili zinanganganiwa huko ziliko, n.k.
ReplyDeleteNi nini kinafukuta??!!