Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge hilo, Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo, Nderakindo Kessy na kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
 Katibu wa wabunge wa Afrika Mashari kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy  na Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa. 
 Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakibadilisha mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Adam Kimbisa, Nderakindo Kessy na Makongoro Nyerere.

Bunge la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake rasmi ambapo sasa kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya  ya Afrika Mashariki.

Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema hayo katika mkutano na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo.

Mhe. Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA, Tanzania pia imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa  kitafanyika mjini Dodoma.

Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es Salaama au Zanzibar.

Amefafanua kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike Arusha, kimoja kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.

Amesema nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha 2013/2014, ndio itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.

Hata hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni vikao vya bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika Bunge.

Mhe. Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu ni kuwa linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.

Naye Katibu wa watanzania, Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo la kujivunia kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya mazungumzo. Hii ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala yanayojadiliwa Bungeni.

Hatua ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka miongoni mwa wabunge wa EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa mwaka mmoja wa fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la pili.

Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.

Vikao vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013 vilikuwa vitano kwa mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika kila baada ya takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Waheshimiwa Wabunge wetu ktk EAC ,Mhe.Adam Kimbisa, Mhe.Abdullah Mwinyi, Mhe. Shy-Rose Bhanji muwaeleze wazi wazi Wabunge wenzenu wa nchi zingine ktk hili dumbana letu Afrika ya Mashariki ya kuwa wasitegemee wakifikiri Watanzania ni Mzee Jangala na kuwa wanaweza kunufaika na Umoja kwa upendeleo wa Upande mmoja hili waondoe vichwani mwao!!!

    1.Muwaeleze ya kuwa Watanzania hawajui sana Kiingereza lakini uwezo wa kiakili wanao tena wa ziada!!!

    2.Muwaeleze ya kuwa kujua Kiingereza cha kubabaisha kama Wakenya sio Kuelimika!!!

    3.Muwaeleze katk Umoja wowote ule mifano Umoja wa Ulaya na mingine Mambo huamuliwa na watu wote na sio Kundi Moja tu na pia, kuwa katika Umoja sio kigezo cha kukubali kila Azimio linalo wekwa mezani!!!,,,kila Mwanachama anahitaji kulinda maslahi ya watu wake.

    HIVYO MUWAELEZE HASA KENYA NA RWANDA TENA KWA KIINGEREZA SAFI YA KUWA ''FEDERATION NEEDS VOLUNTARY WILL OF ALL PEOPLE AND ALSO IS SUBJECT TO force of logic AND NOT logic of force''

    ReplyDelete
  2. Sawa sawa Mdau wa Kwanza muwaeleze Kenya na Rwanda (waviziaji makini)wasitegemee kuneemeka na vyetu na ya kuwa TANZANIA SIO SHAMBA LA BIBI!!!

    ReplyDelete
  3. Ni kweli kabisa Mdau wa juu:

    Hata hiyo Umoja wa Ulaya (EU) pana mambo nchi zingine zinakata katakata ili kulinda maslahi ya watu wao.

    Mfano katika hili 'Dubwana letu' Afrika ya Mashariki kama Mdau wa kwanza anavyosema, wasilete maazimio kama haya hapa chini ni wazi hatuwezi kubali:

    1.Wasijaribu kuomba Uraisi , yaani uwezekano Banyamulenge kutoka Rwanda aweze kuingia Ikulu ya Magogoni, hilo hata kwa Risasi hakuna Mtanzania atakayekubali!!!

    2.Suala la Ardhi, haiwzekani kwa kuwa Sera ya ardhi Tanzania tunayo muda mrefu tu, ni kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali a serikali.

    3.Muungano wa Siasa (POLITICAL FEDERATION) hilo ni gumu kulipata kwa kuwa AINA ZA SIASA KATIKA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI ZINAPISHANA SANA, SIASA YA TANZANIA SIO SIASA YA KENYA NA UGNADA NA VIVYO HIVYO NCHI ZOTE,,,NAWASHAURI WABUNGE WETU EA MUWAELEZE HUKO HILI YA KUWA SHIRIKISHO LA SIASA (POLITICAL FEDERATION ANALO PIGANIA RAISI MUSEVENI WA UGANDA) HALITAWEZEKANA EAC KWA KUWA AINA YA SIASA ZETU KTK NCHI ZETU EAC ZIPO MZUNGU WA NNE!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...