Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Afrika Mashariki, Adam Kimbisa akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana. Kushoto ni Katibu wa wabunge wa Tanzania katika bunge
hilo, Shy-Rose Bhanji, mbunge wa bunge hilo, Nderakindo Kessy na kulia ni Mhe. Makongoro Nyerere.
Katibu wa wabunge wa Afrika Mashari kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji akifafanua jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Nderakindo Kessy na Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania katika Bunge hilo, Mhe. Adam Kimbisa.
Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakibadilisha mawazo baada ya mkutano wao na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Katibu wa Wabunge wa Afrika
Mashariki kutoka Tanzania, Shy-Rose Bhanji, Mwenyekiti, Adam Kimbisa, Nderakindo Kessy na Makongoro Nyerere.
Bunge la tatu EALA limeridhia Tanzania kupata kikao chake
rasmi ambapo sasa kikao kitafanyika Dodoma na vikao vingine viwili kufanyika
Arusha ambayo ni Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwenyekiti wa wabunge wa Tanzania, mhe. Adam Kimbisa amesema
hayo katika mkutano na wabunge watanzania EALA, na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam, leo.
Mhe. Kimbisa amesema katika ratiba ya vikao vya Bunge la EALA,
Tanzania pia imepata rasmi kikao kimoja ambapo sasa kitafanyika mjini Dodoma.
Vile vile amesema kikao hicho kinaweza kufanyika Dar es
Salaama au Zanzibar.
Amefafanua kwamba, Bunge limeridhia vikao viwili vifanyike
Arusha, kimoja kifanyike Tanzania sambamba na nchi zingine wanachama; Kenya,
Uganda, Rwanda na Burundi kupata kikao kimoja kila nchi kwa mzunguko.
Amesema nchi ambayo itakosa kikao kwa mwaka huu wa fedha
2013/2014, ndio itakuwa nchi ya kwanza kupata kikao cha mwaka ujao wa fedha.
Hata hivyo amesema, vikao vikao viwili vya Arusha vitakuwa ni
vikao vya bajeti na ukaguzi wa mahesabu ambavyo ni vikao muhimu sana katika
Bunge.
Mhe. Kimbisa amesema kikubwa wananchi wanachotakiwa kufahamu
ni kuwa linapokuja suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Arusha ni Makao Makuu
na kwamba haiko Tanzania kwani nchi zote tano ni wadau wa Arusha.
Naye Katibu wa watanzania, Shy-Rose Bhanji amesema ni jambo
la kujivunia kwamba Tanzania sasa itakuwa na kikao rasmi kwa njia ya
mazungumzo. Hii ni hatua nzuri vile wananchi pia watapata mwamko wa masuala yanayojadiliwa Bungeni.
Hatua ya maridhiano hayo imefuatia mgoghoro ulioibuka
miongoni mwa wabunge wa EALA kwamba vikao vya Bunge hilo vifanyike Arusha kwa
mwaka mmoja wa fedha na si kwa mzunguko kama ilivyozoeleka kuanzia Bunge la
pili.
Wabunge wengi isipokuwa watanzania walitaka vikao viendelee
kwa mzunguko nchini Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Arusha.
Vikao vya EALA hadi mwaka wa fedha June 2012/June 2013
vilikuwa vitano kwa mwaka. Vikao hivyo vimeongezeka kuwa sita. Vikao hufanyika
kila baada ya takriban miezi miwili, kwa kipindi cha wiki mbili.
Waheshimiwa Wabunge wetu ktk EAC ,Mhe.Adam Kimbisa, Mhe.Abdullah Mwinyi, Mhe. Shy-Rose Bhanji muwaeleze wazi wazi Wabunge wenzenu wa nchi zingine ktk hili dumbana letu Afrika ya Mashariki ya kuwa wasitegemee wakifikiri Watanzania ni Mzee Jangala na kuwa wanaweza kunufaika na Umoja kwa upendeleo wa Upande mmoja hili waondoe vichwani mwao!!!
ReplyDelete1.Muwaeleze ya kuwa Watanzania hawajui sana Kiingereza lakini uwezo wa kiakili wanao tena wa ziada!!!
2.Muwaeleze ya kuwa kujua Kiingereza cha kubabaisha kama Wakenya sio Kuelimika!!!
3.Muwaeleze katk Umoja wowote ule mifano Umoja wa Ulaya na mingine Mambo huamuliwa na watu wote na sio Kundi Moja tu na pia, kuwa katika Umoja sio kigezo cha kukubali kila Azimio linalo wekwa mezani!!!,,,kila Mwanachama anahitaji kulinda maslahi ya watu wake.
HIVYO MUWAELEZE HASA KENYA NA RWANDA TENA KWA KIINGEREZA SAFI YA KUWA ''FEDERATION NEEDS VOLUNTARY WILL OF ALL PEOPLE AND ALSO IS SUBJECT TO force of logic AND NOT logic of force''
Sawa sawa Mdau wa Kwanza muwaeleze Kenya na Rwanda (waviziaji makini)wasitegemee kuneemeka na vyetu na ya kuwa TANZANIA SIO SHAMBA LA BIBI!!!
ReplyDeleteNi kweli kabisa Mdau wa juu:
ReplyDeleteHata hiyo Umoja wa Ulaya (EU) pana mambo nchi zingine zinakata katakata ili kulinda maslahi ya watu wao.
Mfano katika hili 'Dubwana letu' Afrika ya Mashariki kama Mdau wa kwanza anavyosema, wasilete maazimio kama haya hapa chini ni wazi hatuwezi kubali:
1.Wasijaribu kuomba Uraisi , yaani uwezekano Banyamulenge kutoka Rwanda aweze kuingia Ikulu ya Magogoni, hilo hata kwa Risasi hakuna Mtanzania atakayekubali!!!
2.Suala la Ardhi, haiwzekani kwa kuwa Sera ya ardhi Tanzania tunayo muda mrefu tu, ni kuwa ardhi yote ya Tanzania ni mali a serikali.
3.Muungano wa Siasa (POLITICAL FEDERATION) hilo ni gumu kulipata kwa kuwa AINA ZA SIASA KATIKA NCHI ZA AFRIKA YA MASHARIKI ZINAPISHANA SANA, SIASA YA TANZANIA SIO SIASA YA KENYA NA UGNADA NA VIVYO HIVYO NCHI ZOTE,,,NAWASHAURI WABUNGE WETU EA MUWAELEZE HUKO HILI YA KUWA SHIRIKISHO LA SIASA (POLITICAL FEDERATION ANALO PIGANIA RAISI MUSEVENI WA UGANDA) HALITAWEZEKANA EAC KWA KUWA AINA YA SIASA ZETU KTK NCHI ZETU EAC ZIPO MZUNGU WA NNE!!!